Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

ASILIMIA 24% YA WAAFRIKA HUTUMIA INTERNET

Takwimu zilizotolewa kwenye majadiliano yanayofanyika kwenye jiji kuu la Rwanda Kigali yameonyesha kwamba matumizi ya internet mpaka sasa miongoni mwa nchi za kiafrika yamefikia kwenye kiwango cha asilimia 24% peke yake.Hii imelifanya bara hilo kusalia nyuma kwa kiasi fulani kutokana na wadau kutofikia hatua inayotakiwa.

Hii ni mojawapo ya changamoto zinazojadiliwa na wadau mbalimbali kwenye sekta ya mawasiliano ya mtandao kiasi kwamba juhudi zinachukuliwa ili simu za mkononi pamoja na internet viweze kuwa chachu ya maendeleo.

Gerald Rasugu, ni mkurugenzi mkaazi anayewakilisha bara la Afrika  kusini mwa jangwa la sahara kwenye kampuni ya kimataifa ya GSM anasema ni lazima juhudi za makusudi zichukuliwe ili mtandao wa intanet uwe msingi wa uchumi endelevu wa mataifa ya kiafrika”Tatizo la mtandao hasa maeneo ya vjijini barani Afrika ni changamoto kubwa, ni lazima kampuni kama ile yetu ihakikishe inabuni mikakati ya kuhakikisha simu za mkononi zinazotumia mtandao wa internet zinapatikana kwa wingi”Alisema Rasugu

Hata hivyo wananchi wamelalamikia pia tatizo la gharama za kutumia mtandao wa simu za mkononi kutokana na kwamba kila kampuni ya simu inavutia kwake kwa sababuza kiushindani.Hata hivyo tatizo hili limetajwa kufikia kikomo kwenye nchi kama Rwanda ambayo inajaribu kujipambanua kama kitovu cha sayansi na teknolojia Afrika mashariki na kati.Na hii ndiyo maana makampuni makubwa ya mawasiliano ya MTN na Airtle nchini Rwanda yakaamua kusaini mkataba wa kuingia ubia”Asilimia 70% ya watumiaji wa simu za mkononi kwenye mtandao wetu, hawana matatizo lakini imetokana na jinsi tulivyowekeza kiasi kikubwa cha pesa ili tuweze kupata mtandao wa kutosha.Tunataka kufikisha internet ya kiwango cha 3G nchini kote ktk kiwango cha asilimia 95% na tukifanikiwa kufanya hivyo tunaamini itatatua changamoto zinazopatikana kwa sasa” Alibaini Bart Hofker mkurugenzi mkuu wa MTN Rwanda

Takwimu pia zimeonya kwamba watu miliyoni 774 kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika ndiyo wanaomiliki simu za mkononi, wakati watumiaji wa internet ni teluthi moja ya idadi hiyo. Wadau hawa wanasema na sera zinazowekwa na serikali za mataifa husika zimekuwa hazikidhi mahitaji ya wakazi wake wenye kuhitaji huduma hii wakati ndiyo ingekuwa mkombozi mkuu kwenye suala la hili ambalo baadhi ya mataifa miundo-mbinu ya barabara bado ni changamoto kubwa.

@Rwandaleo

Maoni Husiano

Mchungaji mkuu wa kanisa la Anglikani amejitundika

Leki Aimat

Nyamagabe: Raia wanaomba serikali kujenga soko kwa uharaka

Leki Aimat

RWANDA YATHIBITISHA KUMKAMATA SANKARA

Leki Aimat

Toa maoni