Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SIASA SLIDE

Burundi:  212 wapoteza maisha mwaka 2019

Shirika la kutetea haki za binadamu HRW limetangaza kuwa watu 212 wamepoteza maisha nchini Burundi tangu January hadi June 2019.Vifo hivyo vimetokana na visa mbalimbali yakiwemo mauaji.

Ripoti iliyotolewa na shirika hili tarehe 7 July 2019, imetaja kuwa watu 212 ndio wameuwa, ila miili 104 ndio imeshapatikana.

Katika ripoti hiyo pia watuu 29 hakuna anaye jua mahali walipo huko Burundi, 164 walinyanyaswa vikali sana, 468 waliwekwa gerezani kinyume na sheria na wengine 34 wakabakwa.

SOS Media/Burundi imetangaza kuwa kati ya watu 34 waliobakwa, 16 kati yao ni watoto wenye umri chini ya miaka 18, na baada ya ubakaji waliuawa

Ripoti hii imefafanua pia kwamba kutoadhibu watenda maovu wakiwa wanachama wa chama tawala Burundi, na kufunga vyombo vya utangazaji habari ni mojawapo ya kuficha na kuendejeza wanaotenda unyanyasaji.

@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

RWANDA NI SALAMA KWENYE USAFIRI WA ANGA

Leki Aimat

Mchungaji mkuu wa kanisa la Anglikani amejitundika

Leki Aimat

CYANIKA/RWANDA:WALALAMIKIA HUDUMA MBOVU

Leki Aimat

Toa maoni