Rwanda Leo
Image default
BURUDANI HABARI HABARI KWA UFUPI SIASA SLIDE

China haitaruhusu ndoa za watu wa jinsia moja

China imetangaza Jumatano kwamba haitaruhusu ndoa za watu wa jinsia moja, licha ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati kuitaka Bejing kufuata nyayo za Tawain ambayo imeruhusu ndoa za jinsia moja.

Msemaji wa Bunge la China amesema kwamba msimamo wa kisheria wa China unabaki ule ule wa kutambua kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke.

Mwezi Mei 2019 Taiwan ilikuwa taifa la kwanza la Asia kuidhinisha ndoa ya watu wa jinsia moja baada ya mjadala wa miaka mingi juu ya usawa wa ndoa.

Wachambuzi wanasema kuna jamii kubwa ya mashoga katika miji mikubwa ya China.

Katika miezi ya hivi karibuni jamii hiyo imekuwa ikilengwa kwa kuhesabiwa na kuzusha hofu huenda wachina wakaanza kutowastahmilia.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

Wengine 6 wa ajali ya moto wapoteza maisha

Leki Aimat

RWANDA: SHERIA ZA UKOLONI ZAPIGWA MARUFUKU

Leki Aimat

Nyamagabe: Mto wa Mushishito huharibu mavuno ya wakulima

Leki Aimat

Toa maoni