Rwanda Leo
Image default
AFYA HABARI SLIDE

CYANIKA/RWANDA:WALALAMIKIA HUDUMA MBOVU

Taarifa kutoka jimbo la kaskazini mwa Rwanda wilayani Burera zinasema kwamba baadhi ya wagonjwa wametoa malalamiko yao kuhusu huduma mbovu inayotolewa kwenye zahanati moja iliyoko eneo la Cyanika wilayani humo.
Baadhi ya wagonjwa wamekwenda mbali na kutaja kuwa hadi wanakaa siku tatu bila kupata huduma wakiwa kwenye zahanati hiyo.
Venuste Majyambere ni mkazi wa Cyanika, amesema kuwa huduma mbovu inayotolewa kwenye zahanati hiyo inatokana na manesi na wahudumu wengine wa afya kupoteza muda wakiwa kwenye simu zao za mkononi.
 “Nilisikia kwenye radio kwamba wahudumu wa hospitali hawaruhusiwi kutumia simu za mkononi wakiwa kazini lakini hapa wanazitumia kama kawaida bila kuficha, na hawataki kutupa huduma nzuri, unapokwenda wanakwambia urudi kesho yaani hata ukiwa na hali mbaya bado utaambiwa hivyo ” Venuste alisema.
 Emmanuel Nkurunziza ni raia mwingine ambaye pia anailalamikia huduma hii mbovu anasema kuwa siku moja alikuwa mgonjwa akaenda huko na wauguzi walimwambia arudi siku inayofuata, na aliporudi na asipate huduma aliamua kuwaendea wakuu wa zahanati.
Mganga mkuu wa Zahanati ya Cyanika Urimubenshi Francois Xavier amejitetea akibaini tatizo la uchache wa wahudumu , huku hata hivyo akidai kuwa huenda tatizo hilo likapatiwa ufumbuzi bila kutaja ufumbuzi huo kinagaubaga.
Zahanati ya Cyanika kila siku hupokea wagonjwa kati ya 50 na 60 na huduma hii inayotajwa kuwa mbovu imezua visa vya hapa na pale vya wananchi kuvuka nchi ya Ng’ambo kupata huduma ya matibabu.
Peacemaker Etienne Mbarubukeye@rwandaleo

Maoni Husiano

ASILIMIA 24% YA WAAFRIKA HUTUMIA INTERNET

Leki Aimat

Rwanda: Akamatwa na madawa ya kulevya

Leki Aimat

RWANDA: NAFASI YA UFARANSA KWENYE MAUAJI YA 1994

Leki Aimat

Toa maoni