Rwanda Leo
Image default
AFYA SLIDE

Cyarwa: raia waangamizwa na maradhi ya matekenya

Nambali nyingi ya raia wa kiini  cha Cyarwa wameangamizwa na magonjwa ya  matekenya. Rai hawa wanaregea kuwa magonjwa haya waliyarithi kutoka kwa wazazi wao kwa kuwa nao walikuwa na magonjwa haya.

Magonjwa haya ya matekenya yamejitokeza hasa hasa kwenye kiini cha Cyarwa, taarafani mwa Tumba. Rai hawa wana hakikisha kuwa wanajaribu kufanya jinsi wawezavyo ili wafanye usafi lakini wakapatwa na maradhi haya.

Rai wanahakikisha kwamba magonjwa haya waliyarithi kutoka kwa wazazi wao. Moja wapo wa wazazi wao, walitumia kukataa kuwasafisha wakati wakingali wachanga. Wengine wanaregea kuwa magonjwa haya ya matekenya wanayaletewa na uchawi. Wanasema kuwa wenzao wanawapa uchawi wakupatwa na matekenya.

Anateswa na matekenya

Murinda August ni mmoja wapo wa watu walio angamizwa na magonjwa haya. Baba huyu ana umri wamyaka 38. Anasema kuwa alipatwa na maradhi ya matekenya akiwa na umri wa myaka mitanu, lakini anasema kuwa hajui mahali ambapo magonjwa haya yalipo toka.

Eti “mamangu aliaga dunia nikingali mchanga. Kwa hayo, mimi sikua na ujuzi wa kusafisha nyumba. Pia na babangu alikuwa mlevi kwa hayo nilikosa mtu wa kunisaidia kutosha matekenya. Matekenya yaliongezeka hadi leo lakini mimi nadhani kuwa ni uchawi kwa sababu najaribu kusafisha nyumba na kufua nguo zangu lakini inaendelea”

Kabalisa Beatrice, raia wa kiini cha Cyarwa mwenye umri wa myaka 18, naye ni mugonjwa wa matekenya anasema kuwa alipata maradhi haya kwa uchawi.

“Nilipata matekenya kwa uchawi kwa sabubu jirani wetu mtoto wake aliaga dunia kisha aliamua kuwa familia yangu ndiyo imemuua. Baadaye nilipatwa na matekenya  iwapo najaribu kufanya usafi nyumbani mwetu na kufua nguo zangu.”

Ntirurambirwa Damien, Kiongozi wa afya bora ya rai taarafani mwa Tumba, anahakikisha kwamba raia hawa wanapatwa na matekenya kutokana na itikadi zao za kuamua kuwa ni uchawi. Kusema kuwa waliyarithi kwenye familia zao iwapo wangeweza kuwa na usafi.

“namba za watu ambao wako na magonjwa ya matekenya ilipunguzika lakini hao wanaobaki nao ni kwa sababu ya itikadi ya kusema kuwa matekenya yanaletwa na uchawi pia nakuyarithi kutoka kwa wazazi wao. Mtu harithi matekenya cha kwanza ni usafi kama kufagia nyumba.”

Damien ameongeza kuwa wameenda kufanya wawezavyo ili wafundishe raia hawa kuwa na usafi ili tatizo hili walitafutiye dawa ya muda mrefu ya kumaliza suala hili katika taarafa hiyi.

Tumba ni moja wapo ya taarafa zinazo unda wilaya ya Huye. Pia ni taarafa inayo na masuala tofauti kama matekenya, miimba zaharamu na namba nyingi ya washerati.

Tatizo la matekenya linapatikana katika Tarafa hiyi iwapo serikari ya Rwanda ilifanya iwezavyo ili raia wawe nausafi kama kulala kwenye godora na kutengeneza nyumba vyema kwa kutumia udongo ili viloboto visipatikane kwa kuwa viloboto vinaletwa na uchafu.

 

Athanase Munyarugendo@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Centre Africa: Serikali  na Wapinzani wake wamesaini makubaliano ya amani

Leki Aimat

RWANDA: MIKUTANO YA KIMATAIFA  CHACHU YA MAENDELEO

Leki Aimat

CYANIKA/RWANDA:WALALAMIKIA HUDUMA MBOVU

Leki Aimat

Toa maoni