Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SIASA SLIDE

DRC: Baada ya miezi 7 baraza la mawaziri latangazwa

  • Rais Félix Tshisekedi atangaza baraza jipya la mawaziri katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Serikali ya kwanza ya rais Félix Tshisekedi imetangazwa leo Kinshasa, baada ya kusubiriwa kwa miezi saba.

Katika serkali hio mpya, wanawake wanapewa asilimia kumi na saba ya mawiziri na wanaume asilimia 83. Taarifa husema kua kuna sura mpya katika baraza hilo jipya la mawaziri ambazo hazijawahi kuwepo katika serikali.

Kadhalika kumeundwa wizara maalum ambayo itashughulikia watu wenye ulemavu.

Serkali ya muungano ina jukumu la kuimarisha usalama nchini na kuboresha maisha ya raia wa DR Congo.

Mnamo Julai mwaka huu Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikubaliana kuunda serikali ya muungano.

Walikubali kuunda serikali itakayo kuwa na mawaziri 66. Kama walivyo kubaliana, chama cha rais huyo wa zamani sasa kimepata wizara 43, na kile cha rais Félix Tshisekedi kimejinyakulia wizara 23.

Maswali yaliulizwa wakati huo huku kukiwa na madai kwamba bwana Tshisekedi alifanya makubaliano ya kugawana mamlaka na bwana Kabila kabla ya uchaguzi huo.

Mashauriano yamekuwa yakiendelea kati ya vyama vyao na na pande hizo mbili zilieleza kwamba mashauriano hayo yatapokamilika serikali itatangazwa.

Miezi sabaa hii leo baadaye sura mpya hiyo ya mawaziri, inayounda serikali ya Kinshasa imetangazwa rasmi.

 

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

Serikali kutumia nguvu kuwaondoa watu kwenye maeneo ya miteremko

Leki Aimat

Naongoza Uganda kama jamaa yangu-Raisi Museveni

Leki Aimat

Mombasa: Gavana Hassan Joho amewapeleka kotini wanasiasa 4

Leki Aimat

Toa maoni