Rwanda Leo
Image default
HABARI SLIDE

DRC: YAIGA RWANDA KWENYE USAFI

Baadhi ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hasa kwenye jiji kuu la nchi hiyo Kinshasa wametangaza utayari wao wa kuiga mfano wa Rwanda katika kuhakikisha jiji lao linakuwa nadhifu kama jiji kuu la Rwanda la Kigali.

Ni baada ya mwezi mmoja baada ya ziara yao nchini Rwanda ambapo walishiriki shughuli zinazofanyika nchini Rwamda kila mwishoni mwa mwezi zinazolenga kufanya usafi maeneo mbalimbali.

Ni shughuli ambazo hufanyika kuanzia  ngazi ya uongozi wa ofisi ya Rais  hadi ngazi ya shina. Ni zoezi ambalo mpaka sasa limeifanya Rwanda kuendelea kuwa kileleni katika suala la usafi unaoshuhudiwa katika kila kona ya nchi.

Mmoja wa wakazi wa jiji kuu la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kinshasa anayemiliki kampuni ya usombaji taka Bishop Josee Rashidi  anasema kwa kutumia mfano wa Rwanda watafika mbali.

‘’Nia yetu ni kuiona Kinshasa iliyo nadhifu kama vile ilivyo Rwanda’’ alimwambia mwandishi wetu jijini Kinshasa.

Mapema mwezi Machi akishirikiana na wananchi kwenye shughuli hizo za usafi maarufu kama  umuganda jijini Kigali eneo la Kicukiro Rais Paul Kagame aliwapongeza wageni hao kutoka Kinshasa akasema huo ulikuwa ni ushahidi wa jinsi waafrika wanavyopaswa kushirikiana kwa kila jambo

‘’Ushirikiano ndiyo tunautaka,Rwanda, Afrika mashariki, kwa sababu ndiyo utamaduni wetu sisi kama waafrika na wanyarwanda kwa ujumla’’

Wakazi hao wa Kinshasa wanasema hawatatulia hadi wameliona jiji lao linakuwa na usafi wa hali ya juu.

Hii imejiri siku chache baada ya shirika la ndege la Rwanda, Rwandair kuanzisha safari za moja kwa moja kutoka Kigali hadi Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo suala ambalo wadadisi wa masuala ya uchumi wanasema litakuwa chachu ya maendeleo na uchumi wa mataifa hayo mawili jirani.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

DRC: Kisa cha Ebola chathibitishwa mjini Goma

Leki Aimat

LINDA MOYO WAKO KULIKO YOTE UYALINDAYO

Leki Aimat

RWANDA YATHIBITISHA KUMKAMATA SANKARA

Leki Aimat

Toa maoni