Rwanda Leo
Image default
INJILI SLIDE

e ni kweli kwamba mhubiri anayefananishwa na Yesu Kristo amefariki?

Michael Job, mhubiri wa Marekani na muigizaji ambaye hivi majuzi alizuru Kenya na kuitwa ‘Yesu bandia’ hajafariki kama ilivyoangaziwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania na Kenya.

Kulingana na uchunguzi wetu jamaa huyo yupo hai na mzima wa afya.

Kadhalika, mhubiri huyo yupo nchini Kenya na kwamba hajatimuliwa kama ilivyodaiwa na vyombo hivyo vya habari.

Inadaiwa kwamba alifariki siku chache tu baada ya kutembelea taifa hilo la Afrika mashariki baada ya kuuguwa ugonjwa wa mapafu.

Hata hivyo mhubiri huyo ameendelea kupakia mtandaoni picha na video ya shughuli zake siku baada ya siku.

Picha na video za karibuni zaidi alizipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook saa nne usiku wa kuamkia leo.

Katika chapisho hilo na kanda za video alizoweka katika akaunti yake ya facebook Bwana Job anaonekana katika gari moja akihubiri Kiingereza huku akisaidiwa na mkalimani huku watu wakifuatilia mahubiri yake.

Aliandika: Leo mimi na Paul Maurer tulipata fursa ya kuhubiri juu ya gari la CFAN . mamia ya watu walifanya uamuzi wa yesu kuwa muokozi wa maisha yao. watoto wengi walimkaribisha Yesu na

Katika chapisho lake katika ukurasa wake wa facebook siku ya Jumatatu, muhuburi huyo aliandika: Ahsante Marc na Catrice mioyo yenu na utumishi wenu na Ahsanteni kwa kuja Kenya! Mungu aliwatumia ninyi kuokoa maisha ya watoto wengi. Kuhubiri Ukristo kwa masikini , kuwaponya wale waliovunjika moyo kuwaachilia waliotekwa, kuwafungulia waliokandamizwa, kuwaponya wengi na kuwaleta wengi karibu katika moyo wa Yesu. Ahsanteni kwa kanisa lenu na urafiki wenu. Waombeeni watu hawa wa Mungu! Tumsifu bwana! Nendeni duniani ili kuhubiri neno kwa viumbe vyote .Nenda ukahubiri injili kwa mtu hii leo. Mungu atakupatia ujasiri huu unavyozungumza . Anakusubiri. Ubarikiwe Ahsante kwa kutuombea, source:bbcswahili

 

@Rwandaleo

Maoni Husiano

DRC: Baada ya miezi 7 baraza la mawaziri latangazwa

Leki Aimat

Jina ulilopewa linaweza kuathiri tabia yako

Leki Aimat

Kigali: Mfanyakazi wa ndani amteka nyara mtoto wa miaka miwili  

Leki Aimat

Toa maoni