Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SIASA SLIDE

Elimu na afya kupewa kipaombele  kwenye  mkutano  wa SDGs Afrika

Baada ya kipindi cha miaka mitatu  barani Afrika  mataifa   yakiweka kivitendo   malengo ya milenia, jumla ya vipengele 17 vya maendeleo  The Sustainable Development Goals Center  (SDGS),  nguvu nyingi  zitaelekekezwa katika sekta ya elimu, afya na kilimo, ambapo inaarifiwa kuwa  zitakuwa chachu ya nguzo zingine.

Rwanda ni mwenyeji wa  mkutano kuanzi Juni 12-14/2019,  ukiwa na lengo la kujadiliana yaliyofikiwa kwa muda wa miaka 3 iliyo malizika,  changamoto  zilizopatikana  ili zitafutiwe ufumbuzi  na kufikia malengo ya miaka 12 inayobaki.

Mkurugenzi mkuu  wa  SDGS Dr Belay Begashaw akiwa na makao yake mjini Kigali,  amesema kwamba bara la Afrika bado liko nyuma kimaendeleo ambapo  asilimia  40 ya wananchi  ndio wanaotumia  umeme wakati asilimia 42 wana tatizo la lishe mbaya pia wakiwa kwenye umasikini.

Mkurugenzi mkuu  wa  SDGS Dr Belay Begashaw amesisitiza kwamba  kuna vitu muhimu vinavyotakiwa kufanyiwa kazi katika SDGS  mfano  katika sekta ya afya, elimu na kilimo, kuwa na chakula, huo ndio msingi. Amesema na hapa namnukuu ’’Hata tukifikia malengo mengine ya  SDGS  lakini  tusipofanikiwa kuwa na elimu pamoja  na afya hakika tutakuwa hatujafikia maendeleo endelevu’.

Septemba 2015, umoja wa mataifa uliweka vipengele 17 vya maendeleo.  Malengo haya yanajumuisha hasa sekta za maendeleo  ya uchumi ili kutokomeza  umasikini, kuimarisha  uhusiano mwema na kuheshimiana  kati ya mabara vile vile kuwa na ushirikiano  bila kutenga  hata mmoja .

 

Christopher Karenzi@Rwandaleo

Maoni Husiano

Rwanda yawasilisha ombi la DRC kuingia EAC

Leki Aimat

Tanzania: Wanafunzi 400 wanashiriki darasa moja

Leki Aimat

Jina ulilopewa linaweza kuathiri tabia yako

Leki Aimat

Toa maoni