Rwanda Leo
Image default
BURUDANI HABARI SLIDE

GICUMBI: WAWILI WAPOTEZA MAISHA

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 70 kulazwa hospitalini baada ya kunywa pombe ya kienyeji wilayani Gicumbi Kaskazini Mashariki mwa Rwanda.

Tukio hilo lilitokea jumamosi iliyopita baada ya watu zaidi ya 100 kukusanyika katika nyumba ya familia moja kwa lengo la kuhudhuria khafla fupi ya kumpokea mtoto mchanga aliyezaliwa wilayani Gicumbi Kaskazini Mashariki ya Rwanda.

Katika khafla hiyo kila mtu aliyeonja pombe hiyo hali yake ilibadilika ghafla, kiasi cha mtu mmoja kupoteza maisha papo hapo mwingine akafariki akiwa tayari hospitalini na wengine sabini wamelazwa.

Daktari mkuu wa wilaya ya Byumba ameeleza miongoni mwa vitu ambavyo hu1enda vimesababisho vifo hivyo.

Hii si mara ya kwanza nchini patokee vifo vya namna hii na serikali ya Rwanda imekuwa ikiwasihi watu kuacha kutengeneza pombe za kienyeji kiholela.

“Nilianza kuumwa tumboni na nilikuwa nahisi baridi kali mno nikitetemeka huku kichwa kikiniuma zaidi, nilipofikishwa hapa nasikia nafuu sana isipokuwa mgogo pekee ndiyo unaoniuma”

Amesema mmoja wa waathirika.

 

@rwandaleo

Maoni Husiano

Kwa maana ndani yake yeye tunaishi

Leki Aimat

RAIS KAGAME AWAPANDISHA VYEO ASKARI 16 WA JESHI LA ANGA

Leki Aimat

RWANDA: QATAR NA RWANDA ZAZIDISHA USHIRIKIANO KWENYE SEKTA YA SHERIA

Leki Aimat

Toa maoni