Rwanda Leo
Image default
AFYA HABARI

Huye: Utapiamlo ungali changamoto

Tatizo la utapiamlo kwenye tarafa ya Tumba limetajwa na baadhi ya wananchi kuwa changamoto katika maisha yao ya kawaida. Raia hao wamesema kwamba tatizo kubwa ni la viongozi wao ambao wameshindwa kuwa karibu nao kuwapa maarufa kuhusu jinsi ya kupambana na utapiamlo.Mmoja wao Paul BIZIMANA, mkazi wa kijiji cha Rimba anasema kuwa  wanapohitaji kuwaona viongozi wao hawaonekani kwa urahisi.

“ Hatuna mkutako wowote katika siku za kawaida, isipokuwa wakati wa shughuli za  ujumla (umuganda rusange), ili tuzungumze kuhusu saula fulani inayohusiana na jamii yetu.” Paul Bizimana anasema mkazi huyu.

Haya  pia  yanasisitizwa na Mukeshimana Laurence ambaye ametaja  kuwa  kila siku viongozi hao wanakuwa katika biashara yao na hawapati nafasi ya kujadiliana na raia kuhusu changamoto mbalimbali.

Hata hivyo kauli hizi zimekanushwa vikali na viongozi hao. NTIRURAMBIRWA Damien ni katibu wa kijiji hicho“ Tuna mikutano mingi na raia wetu. Sijui ni kwa nini wakazi hao wanasema kuwa  hawapati viongozi. Kila siku tunawafundisha kuhusu maisha na namna ya kuhudumia watoto wao”.

 

Ndisanze Ildephonse@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

RWANDA NI SALAMA KWENYE USAFIRI WA ANGA

Leki Aimat

Elimu na afya kupewa kipaombele  kwenye  mkutano  wa SDGs Afrika

Leki Aimat

RWANDA: RAIS KAGAME AKIRI KUNA DOA KATI YAKE NA UGANDA

Leki Aimat

Toa maoni