Rwanda Leo
Image default
BURUDANI HABARI HABARI KWA UFUPI SLIDE

Jina ulilopewa linaweza kuathiri tabia yako

Kila binadamu ana jina ambalo aliitwa wakati alipozaliwa, lakini unafahamu kuwa jina ulilopewa linaweza kuathiri tabia yako, wanasema wataalamu

Ni dhahiri kwamba hakuna kiumbe kisichokuwa na jina, iwapo kiumbe hicho kiliumbwa wakati dunia ilipoanza au hata kimebuniwa hivi karibuni mfano vile vitu vilivyoumba kiteknolojia, mithili ya binadamu na vinginevyo.

Lakini Je ni watu wangapi wanajua maana ya majina yao au hata kile kilichopelekea wao kuitwa majina hayo na ni vipi jina linaweza kuathiri tabia ya mtu?.

Jamii nyingi awali zilikuwa zikiwapa majina watoto kulingana na majira, nyakati, misimu ambayo watoto hao wamezaliwa au namna mtoto alivyozaliwa.

Hata hivyo kuna baadhi ya jamii ambazo ziliwapatia watoto majina ya mababu. Lakini hata hivyo mtu ambaye angetajiwa jina lazima angekuwa ni mtu ambaye jamii ilitambua maadili yake, mfano mtu ambaye alifariki kwa kujiua alipewa jina fulani.

 

Aggrey ondiege anatoka katika kabila la Luo Magharibi mwa Kenya. Watu kutoka kabila lake huchanganya nyakati na majira.

“Katika kabila letu walikuwa wakitumia wakati kumpatia mtoto jina la kwanza… Kama mtoto amezaliwa, asubuhi au mchana. Kama amezaliwa mchana anaitwa Ochieng akiwa mvulana ama Achieng akiwa msichana. Pia tuliwapatia majina kulingana na majira. Wakati wa mvua au ukame. Tulichanganya majina ya wakati na yale ya majira. Kwa mfano Okinyi au Akinyi wakati wa mvua. Kwa hivyo kama mtoto msichana angezaliwa wakati wa mchana na katika majira ya mvua angeitwa Achieng Akinyi”

Jamii hii hutumia silabi “a” kuanza jina la watoto wasichana na “o” kwa watoto wavulana.Hata hivyo namna mtoto alivyozaliwa pia hutumiwa kama kigezo cha kumpatia mtoto jina.

“Kama mtoto amezaliwa kifudifudi angeitwa Awino ama Owino. Namna ya kuzaliwa ilitumiwa kumpa jina.”

Watoto mapacha katika jamii hii hupewa majina teule kulingana na nani anatangulia kuzaliwa.

“Watoto wanaotangulia kuzalliwa kama ni mvulana ataitwa Opiyo, kama ni msichana ataitwa Apiyo na mtindo huu hutumiwa pia na jamii ya Waluhya nchini Kenya ambapo Pacha anayetangulia huitwa Mlongo na wa pili huitwa Mukhwana.

 

@RwandaLeo

 

Maoni Husiano

Makanisa mengi ya leo hayana waaminifu kama Kelebu

Leki Aimat

Rais Felix Tshisekedi Yoweri Museveni waweka mifumo madhubuti ya ushirikiano

Leki Aimat

Abdel Fattah al-Sissi, mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika

Leki Aimat

Toa maoni