Rwanda Leo
Image default
SIASA SLIDE

Kenya: Magaidi 3 wa Tanzania wahukumiwa miaka 15

Watanzania watatu wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 15 kila mmoja baada ya kukutikana na kosa la ugaidi nchini Kenya. 

Wote watatu ni kutoka visiwani Zanzibar, kisiwa kinacho jitawala, walikamatwa mwaka 2018, katika mpaka wa kaunti ya Wajir, upande wa kaskazini mashariki ya Kenya wakijaribu kuvuka mpaka kuingia Somalia. Wahalifu hao walipatikana na baadhi ya vifaa ambavyo vinatumika katika vitendo vya ugaidi.

Mbarouk Ali Adibu (34), Idarous Abdirahman (32) and Islahi Juma (22) waliletwa mbele ya Hakimu Mkazi wa ngazi ya juu Amos Makoros ili hukumu itolewe Jumatano baada ya watu hao kukutikana na makosa siku ya Jumanne. Hivi sasa watatumikia kifungo chao huko katika gereza la Wajir.

Hukumu hiyo imekuja wakati serikali ya Kenya ikiongeza juhudi zake kupambana kupambana na ugaidi kufuatia shambulizi Sehemu ya Biashara na Hoteli mjini Nairobi uliouwa watu 21.

Photo Al Shabab iternet

Kaunti ya Wajir imekuwa ikikabiliwa na athari za mashambulizi ya ugaidi na imekuwa mara nyingi ikitumika kama kituo cha kusajili magaidi kwenda kujiunga na wapiganaji wa kikundi cha Al Shabaab. Chanzo:voa

Maoni Husiano

Sala ya toba ni nini?

Leki Aimat

Rimba: raia wanahitaji mkusanyiko wa wazazi urudishwe

Leki Aimat

LINDA MOYO WAKO KULIKO YOTE UYALINDAYO

Leki Aimat

Toa maoni