Rwanda Leo
Image default
HABARI INJILI SLIDE

KUABUDU KUNAKOKUTANISHA NA MUNGU 1.

IBADA imebeba vitu vingi kuna kusifu na kuabudu, kuomba , matoleo n.k ,hivi vyote viwe vinatukutanisha na Mungu. (unaweza kwenda kuabudu kumbe ukaabudu BURE kusikokutanisha na Mungu.

Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao Akili zao, kwa kutumiwa zimezoezwa kupambanua mema na mabaya. Ebr.5;14). VITU VYA KUTUSAIDIA ILI TUKUTANE NA MUNGU; (A),Kuabudu katika roho,Yohn.4;23-24,1kor.14;1-16, hapa kuna wimbo mpya katika roho na kuomba katika roho. Roho mt. Ndiye anaweza kutusaidia tuimbe katika roho na tuombe katika roho,ms.14-15 katika Wakorintho, nikiomba kwa roho, Nitaimba kwa roho.1kor.14;2,

Ni lugha ambayo Roho mt anakupa ukiomba kwa roho, hakuna anayesikia bali unajijenga nafsi yako, (hasemi na watu bali anasema na Mungu, njia ya kuongea na Mungu ni katika maombi, unanena mambo ya SIRI katika roho yako), Yeye ananena Mungu anafanya kitu ndani yake, ms 4,14,Wengi wamemzimisha Roho, maana hawaelewi lugha, wanataka waombe kwa Akili, watu wamemzimisha Roho ndiyo maana hawaoni nguvu za Mungu.

Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu omba, Mungu anaielewa lugha hiyo japo akili zangu hazina matunda. Kama Roho anataka kunena na Kanisa, lazima mtu apewe tafsiri, lakini mara nyingi ni mtu kujijenga nafsi yake, wakati MZURI ni wa kunena kwa lugha (ni lugha ya rohoni siyo lugha za wanadamu zinazoeleweka), wakati mwingine unaanza kusifu Roho mt. Anakuja kwa nguvu roho yako inaomba (wakati mwingine unatamka lugha ambayo huielewi, kumbe wakati mwingine roho yako inamshukuru Mungu au kuombea watu wengine,Rum.8;26, na mwisho wake unamalizia kwa akili ili wengine wapate kuelewa. Maombi ya kuongozwa na Roho mt. Yana nguvu sana kuliko maombi ya lugha za wanadamu, Shetani anaelewa lugha zote kasoro lugha ya mbinguni hiyo alinyang’anywa, hiyo lugha inamchanganya ,  Unaponena kwa lugha unasema na Mungu japo huielewi lakini Roho mt na Mungu wanaielewa. (ebu tuombe kwa roho maana ni burudani hakuna kuchoka wala Shetani kuelewa nini tunaomba.)

Paulo anasema, nitaomba kwa akili lakini nitaomba kwa roho. Kuomba kwa roho na kuimba kwa roho ni VITU vinavyotusaidia KUKUTANA NA MUNGU KTK IBADA ZETU. Utakapoanza kuomba kwa roho , usimzimishe, usiangalie ile lugha maana unajengwa nafsi yako pia unanena na Mungu mambo ya siri, usijizuie, wakati mwingine unaweza ukaanguka nguvu ya mwili na kustahimili ukawa hauna, mruhusu Roho akuhudumie, akutengeneze utu wa ndani yaani kwa raha. Maombi ya kuomba kwa akili yanachosha lakini ukijaa Roho mt huchoki maana ni nguvu ya Roho mt inakukamata. Roho mt ana msaada ktk Ibada zetu, anatukutanisha na Mungu ili tuabudu katika roho na kweli.  Kila HUDUMA unayoifana kama mshirika ni msaada sana, maana ni Mungu mwenyewe, huwezi kutenganusha Mungu Baba, Mwana na Roho mt.

Ni lazima tujae Roho mt. Maana ndiye anayetusaidia tumwone Mungu katika KUABUDU KWETU. Asili tuliyo nayo iko kinyume na Mungu (wana wa Adamu), Adui wako wa kwanza wa kukuzuia katka Ibada usikutane na Mungu ni mwili wako. (kwa asili mwili hautaki Ibada), ndiyo maana tunahitaji Roho mt ili atuwezeshe ktk Ibada zetu tukutane na Mungu.

Yesu aliwaagiza wanafunzi wasitoke mpaka wavikwe uwezo utokao juu. Mdo.1;4-8. Ibada ya kweli ni lazima Roho mt. ahusike. Roho mt. Akitawala unapata UTULIVU wa kuweza kukaa mbele za Mungu. Kuomba ktk roho kunatusaidia tukutane na Mungu, lazima Mungu aonekane, unaweza kuimba kwa roho, ukaimba kabisa wimbo mpya, ukiingia rohoni , Roho anaweza kukupa  wimbo na ukaingia rohoni (anatoa wimbo mpya wala hauhitaji mazoezi.).

 

@Rwandaleo

Maoni Husiano

Kigali: Mfanyakazi wa ndani amteka nyara mtoto wa miaka miwili  

Leki Aimat

Centre Africa: Serikali  na Wapinzani wake wamesaini makubaliano ya amani

Leki Aimat

Huye: Utapiamlo ungali changamoto

Leki Aimat

Toa maoni