Rwanda Leo
Image default
INJILI SLIDE

KUPOKEA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU NA KUJAA ROHO MTAKATIFU.

Bila Roho mtakatifu, Ulimwengu na vyote viujazavyo visingeumbwa (Ulimwengu bila Roho mtakatifu hakuna kitu , mwanzo.1;2–,) Bila Roho mt.Mariamu hasingetungishwa mimba ya Bwana Yesu Luka.1;34-35 ,Bila Roho mt.Yesu asingefufuka,Huduma bila Roho mt.hakuna kitu.

Tusiseme Roho mtakatifu kama nadharia kama Dini zingine. Lazima tujifunze kitu halisi, Agano jipya tuna Neema ya ukuhani, 1petro2;9-10, Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani…..

Utendaji wetu ni tofauti na Mungu, Mungu anatenda kwa Roho wake na sisi inabidi tutende kwa Roho wake.  Jambo la muhimu sana kujua katika utumidhi wetu,Yohana 15;5, pasipo mimi hamwezi kufanya jambo lolote, Anayezaa ni yule anayekaa ndani ya Yesu, Zek.4;6, si kwa uweza wala nguvu bali ni kwa Roho wa Mungu.

(1)Uwezo wa kufanya vitu vikubwa katika ufalme wa Mungu vinapatikana ndani ya Yesu (nje ya Yesu haiwezekani, hakuna namna)

(2)Hakuna uwezekano wa kufanya mambo makubwa katika ufalme wa Mungu bila Kujaa Roho mt. Hapa kuna fumbo, tunapotumika tujue tunatumika katika mazingira gani.

Ukamilifu wa kukaa ndani ya Yesu kuna Mambo mawili;

(a)Kumkiri Yesu (kuokoka kisawa sawa siyo kusema Bwana asifiwe mdomoni maana siku hizi imekuwa ni salamu ya kila mtu), 1Yohn.4;15, Kila akiriye  ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.

(b)1Yohn.4;13, Kushirikishwa Roho mtajatifu. Ujuzi wetu kwamba tuko ndani ya Yesu, Roho wa Mungu anakaa ndani yetu (Tunashirikishwa Roho), Kiroho unapookoka Roho mtakatifu anakuvuta toka dhambini unaingia NDANI YA YESU na YESU ANAKUINGIZA NDANI YA ROHO MT. (anatuchukua na kutuzamisha ndani ya Roho mt. Ndipo Lugha za mbinguni zinaanza kutokea yaani unanena, siyo historia bali ni tendo halisi. Walioelewa Neema hii wakazama ndani ya Roho mt., watakemea pepo na litaondoka mara moja, Upako unavunja Nira, Roho mt. lazima apewe nafasi ili atende kazi.

Yoel;2;28-29,Mungu alianza na Ahadi ya Roho mt. Miaka mingi iliyopita, wote wanaokubali kufanywa makuhani, Mungu anatoa ahadi ya kumimina Roho wake, ni haki yako kila anayemkubali Yesu.mdo.5;32, Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote WAMTIIO.Roho mt. Akiondoka ni kutumia nguvu nyingi mafanikio kidogo. Leo hii Makanisani kuna migawanyiko, waliokoka hivi karibuni lakini hawajajazwa Roho mt,  ,na wengine wa zamani lakini wamekauka, na wengine mpaka wachochewe kama gari liwake (ndipo wanene kwa lugha, bila hivo hakuna kunena), na wengine wamejaa hata anapotembea njiani ananena au anaimba kwa Roho.Ezek.47;1, mto mkubwa usiovukika, utaogelea na kuogelea wala hatamaliza, mdo.1;4-5, Yesu alisema msiondoke, Efes.5;18,mjazwe Roho, Mwamini kwa mara ya kwanza anabatizwa kwa Roho.

Pili uendelee kujazwa baada ya ubatizo, efes.5;28, kubatizwa na kujaa ni vitu viwili  tofauti japo watu wanachanganya.,Visima vilivyofukiwa lazima vizibuliwe, Isaka alivifukua visima vya baba yake Ibrahimu. Mzo.26;18-22.Unaweza kuomba kwa Roho kwa masaa ya kutosha siyo profession, ni mapenzi ya Mungu kila aliyeokoka apokee Roho mt. na anene kwa lugha.

Mia kwa mia.Ikor.14;1-19, Mwamini akiisha kubatizwa kwa Roho anatakiwa aendelee kujaa na kujaa mpaka hata wakina Petro vivuli vyao viliponya watu. Lk.11;14 Mungu atazidi sana kuwapa Roho wake wamwombao? Mdo.2;4–,wote 1. wanafunzi walimpokea Roho kwa sababu ilikuwa ni ahadi, Roho mt. anaweza akaja mwenyewe bila kuombewa na mtu yeyote pia anaweza akaja kwa kuwekewa mikono na mtu aliyejazwa tayari.mdo.19;6, sio lazima uombewe Yesu hakuweka mipaka swala ni kuamini na kuwa na kiu. Jinsi gani utapokea ni maamuzi ya Yesu, Yesu anaondoa viambaza, maamuzi yako kwa Yesu anayejaza, Mungu haangalii Jiografia, wengine hawajazwi kwa sababu ya dhambi za siri, wengine wana woga wa kujaa, wengine wanatumia akili, anaingiaje, kwa kupitia wapi, sikio au? Vizuizi usiviruhusu, cha msingi Yesu anapenda ujazwe.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

WAKIMBIZI WA LIBYA WAWASILI RWANDA

Leki Aimat

LINDA MOYO WAKO KULIKO YOTE UYALINDAYO

Leki Aimat

Rais Kagame aeleza mwelekeo mpya wa ushirikiano na Ufaransa

Leki Aimat

Toa maoni