Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

KUWENI MFANO BORA-KAGAME AYAASA MAJESHI

Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni amirijeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi hiyo amewaasa maafisa wakuu wa jeshi la nchi hiyo kuwa mfano bora katika utendaji kazi.

Rais Kagame ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza jimbo la mashariki mwa Rwanda kwenye wilaya ya Bugesera kwenye chuo cha kijeshi cha Gako ambapo alitoa hotuba kwa maafisa wakuu wa jeshi la nchi hiyo lengo likiwa ni kujadiliana nao mambo kadha wa kadha kuhusu ulinzi na usalama wa Rwanda.

Kongamano kama hili ambalo safari hii limehudhuriwa na maafisa wa jeshi zaidi ya elfu moja hufanyika kila mwaka na huwa ni wakati muafaka uongozi wa jeshi la Rwanda kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na amirijeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama akiwa Rais wa Jamhuri Paul Kagame.

Kagame amewaasa wanajeshi kwa ujumla kusimama kidete katika kutetea maslahi ya taifa hasa kwenye suala la usalama.Lakini pia akasema wanajeshi hao hao wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanashiriki shughuli zinazolenga maendeleo endelevu ya taifa.

”Ninyi ninaowaambia hapa na wengine walio na majukumu kama haya, wote tuna jukumu moja tu la kufanya yaliyo bora.Na kumbuka haya mema ninayoyazungumzia kabla ya kuwafikia wananchi wengine yanaanzia kwenu ninyi”

Rais Paul Kagame amesema kwamba mambo yakiharibika kwenye uongozi wa jeshi basi na mahali pengine hayatakwenda vema.

” Ikiwa mambo hayataenda vizuri kuanzia na sisi tulio hapa basi mjue wazi kwamba hata kwa wananchi wengine hatakwenda vema”

Kongamano la aina hii ndilo kubwa katika ngazi ya jeshi la Rwanda na mambo mbalimbali tena mazito kuhusu uongozi na utendaji kazi wa jeshi huchukuliwa kwenye kongamano hili.

Ni kongamano ambalo huhudhuriwa na waziri wa ulinzi, mkuuwa majeshi ya ulinzi,wakuu wa vyuo vya kijeshi na maafisa wengine waaandamizi kwenye jeshi la Rwanda.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

Rwanda: Msanii shoga wa nyimbo za injili atalindwa kama raia wengine

Leki Aimat

Kigali: Ashtakiwa Kumbaka Mwenye Ulemavu Wa Akili

Leki Aimat

Rwanda: Waziri wa sheria kapigwa faini na trafiki

Leki Aimat

1 Maoni

Gabriel Zakaria TBC February 7, 2019 at 3:35 pm

Hongereni kwa kuanzisha jukwaa hili la habari.

Msomaji kutoka Tanzania.

Jibu

Toa maoni