Rwanda Leo
Image default
HABARI INJILI SLIDE

Kwa maana ndani yake yeye tunaishi

Matendo 17:28

28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

Bwana Yesu asifiwe sana.

Kazi mojawapo ya Yesu msalabani ni kutununua na kutufanya kuwa watoto/wana wa Mungu.

Yohana 1:12

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.

Hivyo utakubaliana nami kuwa baada ya dhambi kuingia duniani tulipoteza uthamani wetu mbele za Mungu alietuumba, lakini Mungu kwa upendo wake aliamua kumtoa mwanae wa pekee ili atununue na kutuzaa upya ndani ya ufalme wa Mungu.

Japo kuwa mwanadamu yeyote yule anaeishi damu ya Yesu ilishamnunua pale msalabani lakini pamoja na hayo bado mwanadam anatakiwa kumkiri Yesu kwa kinywa na kuamini moyoni mwake kuwa alikufa kwa ajili yake ili aweze kupata kibali na haki ya kutembea na kuishi ndani ya Kristo kama mwana wa Mungu na mwenyeji wa ufalme wa mbinguni.

Ukisoma vizuri huo mstari wa Matendo 17:28 Utaona vitu vikubwa vilivyotokea baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu.

Kati ya vitu hivyo ni

  1. Kutuwezesha Kuishi ndani ya pendo la Mungu.
  2. Kutusaidia na kutuongoza Kwenda na kutembea katika mapenzi na makusudi ya Mungu.
  3. Kutupa Kuwa na uhakika wa uhai wetu ktk ulimwengu huu na ule ujao.

Haya yote tunakuwa na uhakika nayo kutokana na jambo moja kubwa alilolifanya Yesu pale msalabani, la kutununua kwa damu yake na kutuzaa kwa upya ndani ya ufalme wa Mungu.

Lakini unachotakiwa kufanya ili kuweza kuishi ktk mpango huu wa Mungu kupitia Mauti na Damu ya Yesu ni Kuzidisha imani yako uliyonayo ndani ya Yesu kwani imani ndicho kitu pekee cha kutusaidia kuishi, kutembea na kuwa na uhai wetu ndani ya Kristo.

Ukisoma ktk Warumi 1:17 inasema:-

Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.

Mwenye haki kwa Mungu ni yupi? Ni yule aliemkiri na kumwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake.

Ni yule ambae anaishi ktk mapenzi na makusudi ya Mungu kwake, na sio kuishi kwa kubahatisha na kufata mkumbo kwa kuiga maisha ya watu wengine( kuishi kwa kufuata mkumbo).

Kwa nini unatakiwa kuishi ktk Kristo Yesu?

Ni kuwa licha ya kuwa na uhakika wa kuishi, kutembea na kuwa na uhai wako ndani yake lakini pia unakuwa na uhakika ya kuwa Mungu anakuwazia mema sana juu yako.

Maandiko yanasema:-

Yeremia 29:11

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Nikwambie kitu.

Usipoteze ofa hii ya Mungu kwako, hebu leo tembea sawasawa ktk nyayo za Yesu, hakika utafanikiwa si tu katika ulimwengu huu bali hata ktk ulimwengu ule ujao, ule uliojaa uzima wa milele ambao Yesu Kristo ndiye mwangaza wake usiku na mchana milele yote.

Nakusalim ktk jina la Yesu, nikikukumbusha kuwa thamani yako nikubwa mno ndani ya Mungu ndio maana alikubali kuruhusu  Yesu afe ili wewe ukombolewe na kuwa huru mbali na mateka ya shetani

Hakika wewe sio mateka tena.

Nakutakia baraka nyingi za Kristo zifunuliwe kwako na hazina zako za gizani Mungu akaziweke wazi mbele yako.

 

@Rwandaleo

Maoni Husiano

RWANDA: SHERIA ZA UKOLONI ZAPIGWA MARUFUKU

Leki Aimat

RWANDA YATANGAZA NOTI MPYA KATIKA SARAFU YAKE

Leki Aimat

DRC: Baada ya miezi 7 baraza la mawaziri latangazwa

Leki Aimat

Toa maoni