Rwanda Leo
Image default
HABARI INJILI SLIDE

LINDA MOYO WAKO KULIKO YOTE UYALINDAYO

LINDA MOYO WAKO KULIKO YOTE UYALINDAYO, maana ndiko zitokazo chemchem za uzima. Mith.4;23, Moyo una ugonjwa wa kufusha, hivyo ni lazima ulindwe usije ukashambuliwa na magonjwa hatarishi, MOYO usipolindwa unafyonza uovu wa kila aina.

Ndiyo maana Mungu anaangalia moyo, je una makorokoro au la! 1Sam.16;6-7, usipolindwa moyo kila utakachosikia kinaingia moyoni na kusababisha majeraha (moyo unajeruhiwa). Moyo usiolindwa unahifadhi:  wivu, uchungu, hila, fitina, uongo, uzushi, ugomvi tena kuna ugomvi wa moyoni, mtu hasemi lakini moyo unagombana na mtu mwingine, matukano na mambo yanayofanana na hayo. Gal.5;20-21, mark.7;21-23, kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

Haya yote yaliyo MAOVU yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. Ndiyo maana Biblia inasema moyo una ugonjwa wa kufisha. Moyo unapokuwa umeumizwa ni rahisi kuvunjika kama glass ya kioo na unakuwa na Ufa. Kitu cha kwanza ,Yesu alichokishughulikia ni mioyo ya wanadamu, alikuja na Tiba ya mioyo, Isay.61;1-2, Royo ya BWANA i juu yangu, ili KUWAGANGA WALIOVUNJIKA MOYO…….,

Je! Moyo utulinde kwa marungu, mapanga, mashoka au mtutu wa bunduki? La! hasha hatufanyi vita ya kulinda moyo kwa jinsi ya mwili bali katika roho, tukiteka kila fikra ipate kumtii Kristo.2kor.10;3-6,Tutalinda moyo kwa ;

(1)Maombi, unapokuwa mwombaji tayari ndipo unaweza kushambulia mishale ya yule mwovu inayokuja kushambulia imani iliyopo moyoni, tunapigana vita katika maombi, tunajenga ukuta imara ili moyo usishambuliwe magonjwa nyemelezi.

(2)Tunalinda moyo kwa kusoma Neno la Mungu kila siku, ndiyo chakula cha roho, Neno ni upanga ukatao kuwili, Ebr.4;12, unaposoma Neno unaingiza upanga moyono ili magonjwa nyemelezi yakija yanakutana na Upanga ukatao kuwili.

(3)Tunalinda moyo kwa kuhudhuria IBADA, ktk ibada kuna mafundisho tunakulia Wokovu tunapata maziwa yasiyoghoshiwa , kuna kuabudu  na kusifu, Mungu hushuka ktk sifa na kutuhudumia mioyo yetu. Hizi ndizo nguzo tatu zinazosimamisha moyo .

Usiingiliwe na Adui akafunga mafundo ya dhambi moyoni. Moyo ukiharibiwa hata mifupa huugua hakuna afya njema natokeo ni magonjwa yasiyo na TIBA, hakuna Uzima. Moyo mbovu huozesha mifupa.

Mwisho: Swala la kulinda moyo ni jukumu la mtu binafsi wala hakuna wa kuchukua hiyo nafasi, sana sana Mungu atatoa watumishi wa kukuelekeza jinsi ya kufanya ili uifuate njia sahihi ya kulinda moyo wewe binafsi wala sivinginevyo. “Bwana atusaidie tuweze kulinda mioyo yetu”.

 

@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

RWANDA: SHERIA ZA UKOLONI ZAPIGWA MARUFUKU

Leki Aimat

RWANDA: WABUNGE WA AFRIKA WALALAMIKIA SERIKALI

Leki Aimat

RWANDA YATANGAZA NOTI MPYA KATIKA SARAFU YAKE

Leki Aimat

Toa maoni