Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI INJILI SIASA SLIDE

MAFUNZO KWA VIONGOZI WAKUU-RWANDA

Rais Paul Kagame wa Rwanda akishirikiana na mchungaji maarufu wa Marekani Rick Waren wamesema baadhi ya mambo kwenye uongozi wa watu na mataifa yanashindwa kwenda vema kutoka na viongozi kukosa mwelekeo.Walikuwa wakizungumza mjini Kigali Rwanda kwenye mwanzo wa semina ya siku mbili kwa viongozi wa serikali na wanadiplomasia wa mataifa ya kigeni nchini Rwanda.

Rick Warren ni mchungaji wa kimarekani anayemiliki kanisa la SaddleBucks la kimataifa. Ni mchungaji na mwandishi wa vitabu maarufu vinavyojikita kwenye masuala ya uongozi wenye malengo.

Amekuwa mjini Kigali Rwanda kutoa mafunzo kwa viongozi wakuu wa nchi hiyo pamoja na wawakilishi wa mataifa ya kigeni nchini Rwanda.

Anasema kwamba dunia imekuwa na matatizo kutokana na baadhi ya viongozi kushindwa kuwa na mwelekeo wa kutekeleza malengo kama yanavyopaswa kuwa.

Ni semina ya siku ambayo imewajumuisha pamoja viongozi zaidi ya 2000 kwa ajili ya kutafajari jinsi ya kuwa na uongozi wenye mwelekeo imara kwa ajili ya mstakabari wan chi ya Rwanda ambayo mchungaji Rick Warren ameitaja kama inayotoa mfano wa kuigwa katika ukuaji wa kiuchumi na uongozi bora wenye taswira ya maendeleo endelevu.

Akizungumza kwa upande wake Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema tatizo si kwamba viongozi hawatambui majukumu yao lakini tatizo kubwa ni kubweteka na kushindwa  kufikia malengo waliojiwekea

‘’ Tunapotoka kanisani, kupata mafundisho na ukifika kule nje ni lazima utafute muda wako utafakari yale uloambiwa na,yaani kila siku, kila wiki au hata kila mwezi, tafuta muda kidogo ujitathmini wewe mwenyewe, ujiulize ukisema lakini, nini ambacho sijakikamilisha, kasoro zangu ni zipi?Na kuanzia hapo upate kutafuta suluhu’’ amesema Rais Kagame

Ni kutokana na kushindwa kujitathmini kwa viongozi kunakosababisha matatizo chungu nzima kwa serikali au hata katika maeneo mengine ya uongozi wamesema.

Rick Warren amesema pia kwamba kutokana na kudiriki kwa viongozi wa Rwanda baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya jamii watutsi kulikoifanya nchi hiyo kupiga hatua ya maendeleo hadi sasa.

‘’Mwaka 1995, mwaka mmoja baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi hakuna mtu hata mmoja aliyehitaji kuja Rwanda, lakini nawaambieni natembea kote barani Afrika kila mmoja kwa sasa anataka kuja Rwanda’’

Semina hii ililenga kuwapiga msasa viongozi wakuu serikalini ili kubadili mienendo na kuitumikia jamii ipasavyo.

 

@Rwandleo.com

Maoni Husiano

MNACHUKULIANA NA WAJINGA KWA FURAHA

Leki Aimat

AFRIKA LAZIMA IWEKEZE KATIKA NGUVU KAZI-RAIS KAGAME

Leki Aimat

RWANDA: RAIS KAGAME AWAASA VIONGOZI DHIDI YA UMASKINI

Leki Aimat

Toa maoni