Rwanda Leo
Image default
AFYA HABARI HABARI KWA UFUPI SLIDE

Mara ya pili kesi ya Ebola imethibitishwa nchini Uganda

Dr. Joyce Moricu Kaducu, waziri wa dola anaeshughulikia huduma za afya ya msingi alithibitisha kesi ya mtoto huyo mwenye asili ya Congo ambaye alikuwa anasafiri na mama yake kuingia Uganda kupitia kituo cha mpakani cha Mpondwe

Wizara ya afya ya Uganda ilithibitisha Alhamis mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa aliyevuka mpaka kutoka Kongo na kuingia Uganda ameambukizwa virusi vya Ebola. Mtoto huyo anapatiwa matibabu kwa wakati huu katika kituo maalumu cha kupambana na Ebola katika wilaya ya Kasese.

Imeripotiwa mtoto huyo alikuwa na dalili za homa kali, pamoja na udhaifu wa mwili, vipele na damu kutoka mdomoni bila ya kufahamu sababu zake.

Damu yake ilipimwa katika taasisi ya utafiti wa virusi vya Ebola ya Uganda na baadae taasisi hiyo ilithibitisha alikuwa na virusi hivyo.

Dr. Joyce Moricu Kaducu alisema binti huyo haraka aliwekwa kwenye chumba cha peke yake na alisafirishwa hadi hospitali ya Bwera kwenye kitengo cha Ebola mahala ambako anapatiwa huduma maalum.

Hii ni mara ya pili kesi ya Ebola imethibitishwa nchini Uganda kutoka kwa waathirika wanaovuka mpaka kutoka Congo kuingia Uganda. Zaidi ya watu 1,800 wamekufa nchini Congo kutokana na ugonjwa huo tangu Agosti 2018.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

Rubavu/Nyarugenge: Wawili wakamatwa katika msako  madawa ya kulevya

Leki Aimat

RWANDA YAANZISHA MAABARA YA KISASA KUPIMA UBORA WA NGUO

Leki Aimat

Rwamagana:Fundi viatu Mwanamke azidi kung’ara

Leki Aimat

Toa maoni