Rwanda Leo
Image default
AFYA SLIDE

Nyamagabe: Raia wanaomba serikali kujenga soko kwa uharaka

Raia wa Nyamagabe wanaitaka serikari kuwasaidia kujenga soko kwa uharaka kwa sababu mahali ambapo serikali iliwapatia mvua imenyeshea bidhaa vyao.

Wilaya ya Nyamagabe ilianza mradi wa kujenga soko la maendeleo, kabla ya kugenga soko hili serikali iliamua kuwatosha wafanya biasha hawa na kuamua kuwapeleka mahali pengine. Raia hawa wanahakikisha kuwa mahali ambapo waliwapeleka, mvua ikinyesha bidhaa vyao huharibika.

Raia hawa pia wanasema kuwa mahali ambapo serikali iliwapeleka pana athiri biashara vyao  kwa sababu wakati ambapo mvua inanyesha inawabidi wakimbie kujikinga mvua na kuacha bidhaa vyao.

Ndagijimana Emmanuel ni mfanya biashara katika soko hili ambapo serikali iliwapeleka, anasema kuwa serikali iliwambia kuwa itajenga soko kwa uharaka kisha warudishwe  kwenye soko la maendeleo lakini ujenzi wa soko hili ulisimama wakati ambapo mvua imenyeshea bidhaa vyao.

Nyiramana Providence naye mfanya biashara katika soko hili ambapo serikali iliwapeleka naye anasema kuwa wakati wa mvua nyingi hawapati wanunuzi wengi kwa kuwa ni vigumu kufika hapo.

Providence eti: “Wakati mvua imenyesha ni vigumu kwa wateja kufika hapa pia wakati ambapo mvua imenyesha tunakimbia tukatupa bidhaa vyetu nje, kwa hayo serikali ingeweza kutusaidia kujenga soko la maendeleo kwa uharaka kisha turudishwe pale”.

Kabayiza Rambert, kiongozi wa Wilaya ya Nyamagabe anaye husika na uchumi anasema kuwa soko lilichelewa kujaa kwa sababu kuna tatizo lilitokea katika ahadi na mtu aliye na kazi ya kujenga soko lakini wameenda kukosoa ahadi ili soko hili lijengwe kwa uharaka.

 

Munyarugendo Athanase@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Tanzania: Wanafunzi 400 wanashiriki darasa moja

Leki Aimat

UWAZI, MAWASILIANO NA TAKWIMU NI MSINGI-RAIS KAGAME

Leki Aimat

Tanzania: Wajumbe wa Rwanda kwenye mkutano wa Umoja wa Africa (ACALAN) Kiswahili

Leki Aimat

Toa maoni