Rwanda Leo
Image default
INJILI

Omba Mungu akupe mabawa kama ya Tai

Tusome katika ufunuo 12:14, neno la Mungu linasema kama yule mwanamuke alipewa mabawa iliyo muruhusu kukimbiliya jangwani ambako alipewa chakula chake mara kwa mara, mbali ya uso wake yule joka.

Katika jangwa tunajuwa kama maisha si raisi hapo, ni fasi ambapo hakuna maji, hakuna chakula, kuna ukavu, jua kali, vumbi la mchanga, na mpepeo kali.  Lakini hata kama maisha ya jangwa ni magumu, pamoja na Mungu jangwa inageuzwa paradizo, kwenye maisha bora, mwanamuke alipata chakula chake mara kwa mara mbali ya uso ya yule joka.

Kwa mwezi huu, Mungu atakupatiya mabawa ili uruke mbali ya shetani, mbali ya shida, mbali ya wachawi, mbali ya mauti, mbali ya magonjwa, mbali ya njaa,  mbali ya umasikini, mbali ya matatizo yote.

 

Alafu utakipata chakula chako kwa wakati unaofaa, mbali ya uso wa maadui wako.

Mabawa utakayopewa ni maombi na neno la Mungu, ambavyo vitakuruhusu kuruka na kujificha jangwani ambako utalishwa mara kwa mara na Bwana Mungu wako.

Tunajuwa kama hata Yesu alijificha jangwani akiomba na kuutafuta uso wa Mungu.

Siku ya leo, mwezi huu, ninawatakiya kupewa mabawa ya tai, ambayo itawaruhusu kuruka mbali na zambi, mbali na shetani, mbali na matatizo.

Mungu awabariki.

Imeandikwa na Ev. Bahati

Rwanda Leo

Maoni Husiano

Sala ya toba ni nini?

Leki Aimat

Kwa maana ndani yake yeye tunaishi

Leki Aimat

Rwanda: Msanii shoga wa nyimbo za injili atalindwa kama raia wengine

Leki Aimat

Toa maoni