Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

RAIS KAGAME AONGOZA KIKAO CHA SMART AFRIKA

Rais Paul Kagame ambaye ni mwenyekiti wa mkakati wa smart Africa unaolenga kuinua kiwango cha matumizi ya sayansi na teknolojia barani Afrika mapema siku ya jumatatu aliongoza kikao cha tume maalum ya mkakati huo kilichofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia.

Smart Afrika ni mpango mkakati unaoundwa na wakuu serikali na marais 12 pamoja na mwenyekiti wa shirika la kimataifa la mawasiliano ITU Houlin Zhao na pia Dr. Amani Abou-Zeid kamishina wa umoja wa Afrika anayehusika na nishati na miundo mbinu.

Rais Kagame amewapongeza wajumbe hao kwa muda wao kuhusu majadiliano ya kuufanya mpango huo kupiga hatua zaidi.Amesema kwamba mpango wa Smart Africa umeendelea kupanuka kwa kuwa mpaka sasa idadi ya mataifa wanachama imeongezeka na kufikia mataifa 24

Aidha, amempongeza mwenyekiti wa ITU Houlin Zhao kutokana na mchango wake mkubwa wa kuhudhuria vikao vya aina hii kila mara anapoalikwa.

Kwa upande mwingine Rais Kagame amempongeza pia Dr Hamadoun Touré ambaye alikuwa mwenyekiti wa Smart Afrika kwa miaka mitatu iliyopita na kusema kwamba mchango wake ni mkubwa ndani ya kipindi hicho.

“Natumia nafasi hii kumpongeza Dr Touré kutokana na kazi yake ndani ya miaka mitatu iliyopita, anamaliza muda wake na tunampata kiongozi mwingine” amesema Rais Kagame.

Kikao hiki pia kimemteua Lacina Kone kutoka Ivory Coast kuwa mwenyekiti wa mpango wa Smart Afrika.

Kikao hiki pia kimehudhuriwa na Rais wa Estonia Kersti Kaljulaid. Hii inafuatia makubaliano baina ya Smart Afrika na serikali ya Estonia yaliyosainiwa mwezi wa tatu mwaka jana ambayo yanalenga kuisaidia Afrika kupiga hatua zaidi kwenye mkakati huu wa teknolojia na mawasiliano.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

RWANDA: QATAR NA RWANDA ZAZIDISHA USHIRIKIANO KWENYE SEKTA YA SHERIA

Leki Aimat

Kigali: Mfanyakazi wa ndani amteka nyara mtoto wa miaka miwili  

Leki Aimat

Huye:Wanafunzi wapigwa msasa juu ya sheria mpya kuhusu rushwa 

Leki Aimat

Toa maoni