Rwanda Leo
Image default
SIASA SLIDE

Rimba: raia wanahitaji mkusanyiko wa wazazi urudishwe

Raia wa Rimba wanasema kuwa viongozi wao hawatii nguvu kwenye mkutano wa mkusanyiko wa wazazi iwapo mkusanyiko wa wazazi huu ulitumia kuwasaidia kufafanua matatizo tofatuti. Viongozi wa tarafa ya Tumba wanahakikisha kuwa wameenda kufanya juu chini ili mkutano huu urudishwe katika kijiji hiki.

Wanao shitaki serikali kutotia nguvu kwenye mkutano wa mkusanyiko wa wazazi ni raia wakijiji cha Rimba, wanahakikisha kuwa mkutano huu umemaliza miezi sita bila kujitokeza kijijini humu. Raia hawa wanajiuliza namna gani jirani wao wana  mkutano huu bila kujitokeza kwao.

Rai hawa wanasema kuwa viongozi wao wangazi za chini wanafanya mambo ya kibinafsi bila kujali faida za jamii. Raia hawa wanasema kuwa mkutano huu ulitumia kuwasaidia kutatua maswala tofauti hasa hasa yanayo jitokeza katika familia zao.

Photo internet

Paul Bizimana ni mzalendo wakijiji cha Rimba anaonyesha kuwa viongozi wao ndio ambao hawasaidii wazalendo kuwa na mkutano huu wa mkusanyiko wa wazazi: “viongozi  wanajali biashala zao bila kujali faida za wazalendo, mkutano huu huwezi kujitokeza iwapo na viongozi hawaonekani. Kinacho kasirikisha raia wa kijiji jirani cha Berwa wanafanya mkutano huu mara mbili katika wiki, tunapo enda kwenye mkutano huu wa jirani wanakataa kutatua matatizo yetu ndiyo maana tunaitaka serikali iturudishie mkutano huu ili nasi tupate maendeleo kama jirani wetu”  Paul asema.

Kiongozi wa maisha bora katika taarafa ya Tumba Damien Ntiruhandurwa, anasema kuwa ni kazi yao ya kuhakikisha kuwa mambo yameendelea vyema katika rai na ndiyo maana wameenda kufanya juu chini ili mkutano huu uludishwe kwa uharaka.

Photo internet

“Tumeenda kufanya jinsi tuezavyo ili mkutano huu urudishwe kwenye kijiji hiki cha Rimba kwa kuwa mkutano huu wa mkusanyiko wa wazazi umetusaidia kutatua matatizo kati yao bila kuyafikisha hapa taarafani” Damienasema

Mkutano wa mkusanyiko wa wazazi uliletwa na serikari ya Rwanda mwaka 2010 kwa kusaidia raia kufafanua matatizo yanayo jitokeza katika familia zao.

Mpango huu umekutana na changamoto tofauti kama pale ambapo watu ambao wanakuja kwenye mkutano huu ni wake tu iwapo uliletewa pia na viume ili kila mtu aonyeshe msada wake katika maendeleo ya kijiji pia matatizo hayawezi kutatua vyema iwako viume hawafiki kwenye mkutano huu.

 

Athanase Munyarugendo@rwandaleo.com

Maoni Husiano

Kwa maana ndani yake yeye tunaishi

Leki Aimat

WAKIMBIZI WA LIBYA WAWASILI RWANDA

Leki Aimat

Sala ya toba ni nini?

Leki Aimat

Toa maoni