Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SLIDE

Russia yaendelea na mashambulizi ya anga

Mashambulizi ya anga yanayofanywa na Russia pamoja na utawala wa Syria yameharibu takribani maeneo yote huko kaskazini mwa Hama na kusini mwa jimbo la Idlib na kuwakosesha makazi watu 800,000 waliopo kwenye mpaka kati ya Syria na Uturuki.

 Taasisi inayofuatilia masuala ya vita na haki za binadamu nchini Syria yenye makao yake Uingereza yaeleza kwamba Serikali ya Syria haijafungua fursa ya msaada wa kibinadamu kwa raia katika jimbo la Idlib huko kaskazini magharibi mwa Syria, ngome ya mwisho ya makundi ya waasi.

Taasisi ya Syrian Observatory for Human Rights inaandika ukiukaji wa haki za binadamu huko Syria ikieleza kuwa tangazo la utawala la kufungua fursa ya msaada wa kibinadamu ni uongo na kwamba hakuna raia aliyeachwa katika eneo ambapo raia wote tayari wameondoka kutokana na mapigano yanayofanywa na vikosi vya utawala.

Rami Abdulrahman mkuu wa taasisi hiyo inayofuatilia masuala ya kibinadamu alisema kuwa njia hiyo imewekwa na Russia na utawala wa Syria kwa ajili ya vyombo vya habari kusema kwamba raia wanakimbia kuelekea maeneo yanayodhibitiwa na utawala wa Syria.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

RWANDA: TEKNOLOJIA CHACHU YA MAENDELEO

Leki Aimat

USALAMA WAHITAJI USHIRIKIANO-INTERPOL

Leki Aimat

MIJI SITA NCHINI TEGEMEO KIUCHUMI

Leki Aimat

Toa maoni