Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI

Rwamagana:Fundi viatu Mwanamke azidi kung’ara

Mama mmoja wilayani Rwamagana mashariki mwa Rwanda ameamua kujibunia ajira ya kushona viatu kutokana na kile anachokitaja kama kuepuka tabia mbaya ya kuwa ombaomba mitaani.Mama huyo(Jina tunalihifadhi) anasema kumekuwepo na tabia ya watu hata wenye viungo vyao kamili kuwa na tabia ya kujifanya ombaomba barabarani kitu ambacho kwa mtazamo wake ni aibu kubwa na kinyume na maadili ya wanyarwanda.

Rwandaleo imepata kujua kuwa mama huyo anaendelea kupiga hatua kwa kasi kutokana na utitiri wa wateja wanaomwendea kwa ajili ya kupata huduma ya kushonewa viatu vyao.

Hata hivyo anasema anaendelea kukabiliwa na mtazamo hasi kutoka kwa wanawake wenzie ambao mara kadhaa wanamsota kidole huku wakitaja kuwa aliamua kufanya kazi ambazo kwa kawaida hufanywa na wanaume.Hata hivyo yeye anasema hilo halimkoseshi usingizi almradi kazi inazidi kupiga hatua.

Baadhi ya wateja waliohojiwa na mwandishi wa Rwandaleo wanasema wanampenda mama huyo kutokana jinsi anavyofanya kazi yake kwa kujituma na kwa uaminifu wa hali ya juu.Kwa mantiki hiyo kuendelea kuwepo kwa mwanamke huyo huenda kukabadili ule mtazamo kuwa baadhi ya kazi ni maalum kwa wanaume na si mtu mwingine.

 

Leki@RwandaLeo.com

Maoni Husiano

DRC: YAIGA RWANDA KWENYE USAFI

Leki Aimat

Sala ya toba ni nini?

Leki Aimat

FAHAMU FAIDA 10 ZA KUOA MWANAMKE MCHA MUNGU

Leki Aimat

Toa maoni