Rwanda Leo
Image default
HABARI SLIDE

RWANDA: BAJETI KWA AJILI YA MATUMIZI YA MTO NAILI

Mataifa yaliyoko kwenye bonde la Mto Nile yamehimizwa kutenga bajeti ya pamoja kwa ajili ya kuhifadhi  maji ya mto huo ambao unayaunganisha mataifa 10 ya Afrika.

Mkurugenzi mkuu wa mradi wa bonde la mto Nile Mhandisi Ntabana Innocent amesema hatua ya kila taifa kuamua kuhifadhi maji ya mto huo kwa kiwango chake na peke yake inapelekea hatari ya uharibifu wa mto huo siku za usoni.

Mhandisi Ntabana Innocent alikuwa akizungumza kwenye mazungumzo na waandishi wa habari jijini Kigali Rwanda kwenye maandalizi ya miaka 20 tangu ulipoanzishwa mradi wa pamoja wa mataifa 10 wa kuhifadhi maji ya mto Nile.

‘’Ikiwa kila nchi itatumia maji hayo kama inavyotaka tutakuwa na matatizo hapo mbeleni.Ni lazima tutafute suluhu jingine  kwa ajili ya kutatua changamoto zitakazojitokeza hapo baadaye kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa”Alisema Mhandisi Ntabana Innocent

Ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita amesema, miradi kadhaa ya hifadhi ya bonde la mto Nile iliandaliwa na kutekelezwa kwa lengo la hifadhi ya maji ya mto huo.

Moja ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi  kwenye maporomoko ya mto Rusumo wenye lengo la kuzalisha nishati ya umeme kwa mataifa matatu  ya Rwanda, Burundi na Tanzania kwa ajili ya kuzalisha megawatt 26.6 za umeme.

 

@Rwandaleo

Maoni Husiano

FAHAMU FAIDA 10 ZA KUOA MWANAMKE MCHA MUNGU

Leki Aimat

CYANIKA/RWANDA:WALALAMIKIA HUDUMA MBOVU

Leki Aimat

UWAZI, MAWASILIANO NA TAKWIMU NI MSINGI-RAIS KAGAME

Leki Aimat

Toa maoni