Rwanda Leo
Image default
HABARI SLIDE

RWANDA: MIKUTANO YA KIMATAIFA  CHACHU YA MAENDELEO

Mamlaka ya taifa inayohusika na kuandaa mikutano ya kimataifa Rwanda Convention Bureau (RCB) imesema kwamba Rwanda imeingiza kiasi cha dola za Marekani milioni 52 katika kipindi cha kuanzia mwezi wa saba mwaka jana hadi mwezi wa kwanza mwaka huu.

Mamlaka haya yamesema kwamba ndani ya kipindi hicho jumla ya wageni  35 000 walitembelea Rwanda kuhudhuria mikutano mbalimbali ya kimataifa.

Serikali imekwishatangaza kwamba kwenye mwaka wa fedha  wa 2018/2019 taifa linatazamiwa kuchuma kiasi cha dola za Marekani milioni 74 zitakazotokana na kupokea mikutano mikubwa na ya kimataifa. Hii ina maana kuwa kiasi cha pesa kitakuwa kimepanda kutoka dola za Marekani milioni 42.

Mkurugenzi mkuu wa RCB Mukazayire Nelly amewaambia waandishi wa habari jijini Kigali kwamba huenda kiasi hicho kilizidi kutokana na njia iliyotumiwa kwenye makadiriyo ya mapato hayo.

Amesema lengo ni kuendelea kuitangaza Rwanda kwenye medani za kimataifa

“Tunataka kuendelea kuitangaza Rwanda, wakati mikutano ya aina hiyo inapofanyika Rwanda mara zote tunajitahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha inakwenda vema ili wageni waendelee kuona Rwanda kama mahali pema pa kutembelea” Amesema Mukazayire

Mamlaya ya RCB hupata ruzuku kutoka serikalini lakini lengo ni kujitegemea ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

Picha: Tamasha la mungu wa kike lavutia wengi

Leki Aimat

UWAZI, MAWASILIANO NA TAKWIMU NI MSINGI-RAIS KAGAME

Leki Aimat

Rubavu/Nyarugenge: Wawili wakamatwa katika msako  madawa ya kulevya

Leki Aimat

Toa maoni