Rwanda Leo
Image default
AFYA BURUDANI HABARI INJILI SIASA SLIDE

Rwanda: Msanii shoga wa nyimbo za injili atalindwa kama raia wengine

Naibu waziri katika wizara ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa,a kihusika na jumuiya Afrika mashariki Balozi Olivier Nduhungirehe amemuambia msanii wa nyimbo za injili, Albert Nabonibo ambaye ni shoga kwamba aendelee na shughuli zake na kuwa serikali itamlinda kama raia wengine.

Nabonibo alikubali kuwa anapenda watu wa jinsia yake yaani kiume.

Hata hivyo, watu kadharika walikuwa wakimkosoa kwa mawazo yao mengi hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa hilo, Waziri Nduhungirehe amesema “ Endelea na shughuli zako za kumuabudu Mola, serikali itakulinda.”

Nabonibo ni msanii wa kwanza nchini Rwanda kutangaza hadharani kuwa yeye ni shoga.

Nchini Rwanda, hakuna sheria dhidi ya ushoga ila sheria inakataza ndoa kati ya watu wa jinsia moja.

 

 

 

@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Wengine 6 wa ajali ya moto wapoteza maisha

Leki Aimat

USALAMA WAHITAJI USHIRIKIANO-INTERPOL

Leki Aimat

KUABUDU KUNAKOKUTANISHA NA MUNGU 1.

Leki Aimat

Toa maoni