Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SLIDE

Rwanda: Mwanamke asema alivyofanya Nchini Kuwait

Mwanamke wa miaka 41, mkazi mjini Kigali ametangaza alivyofanya vitendo vya utumwa nchini Kuwait.

Ameambia vyombo vya habari nchini Rwanda, kuwa hatasahau aliyokabiliana nayo nchini Kuwait baada ya kwenda huko kwa ahadi kwamba atapata malipo ya $ 400.

Amesema alipofika nchini Kuwait, alipokonywa vitambulisho vyake halafu akapewa kazi kupiga deki ghorofa tatu kila siku.

“ Kazi yangu ilikuwa kupiga deki  jumba la ghorofa tatu na kuwalea watoto sita.” Amesema

Alishindwa kazi hii lakini bwana wake akakataa kumuacha kwa  kumuambia “ Nililipa dola elfu mbili na nauli ya ndege, usiniambie hayo.”

Bwana wake alijaribu kumbaka lakini akashindwa. Baada ya tukio hilo, alimpeleka gerezani kwa kuogopa kwamba mke wake atajua.

Serikali ya Rwanda iliwasadia kurudi nchini Rwanda kupitia watu iliyowatuma huko.

Rwanda ilikabiliana na suala la baishara la watu miaka miwili iliyopita. Mwaka 2017, kulikuwepo kesi  47 na 49 mnamo mwaka 2018.

 

@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Ninyi ni uzao wa nyoka, maneno huonyesha hali ya moyo

Leki Aimat

MAONYESHO YA KAHAWA BORA KUFANYIKA RWANDA

Leki Aimat

Rubavu/Nyarugenge: Wawili wakamatwa katika msako  madawa ya kulevya

Leki Aimat

Toa maoni