Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

RWANDA NI SALAMA-WAZIRI WA MASHAURI YA KIGENI

Waziri wa mashauri ya kigeni na msemaji wa serikali ya Rwanda Dr Richard Sezibera amewaasa wanyarwanda kutopoteza muda wakisikiliza habari zinazowapotosha kuhusu usalama wa Rwanda.Siku chache zilizopita nchi za Ufaransa na Canada zilitoa angalizo kwa wananchi wake wanaosafiri kwenda Rwanda kuwa waangalifu wanapokwenda maeneo mbalimba hasa kwenye hifadhi ya wanyama ya Nyungwe na Virunga.

Kwenye tovuti ya wizara ya mashauri ya Ufaransa kuliandikwa ujumbe uliosema kuwa ‘’Kutokana na changamoto zilizopo si vizuri kutembelea hifadhi ya wanyama ya virunga’’

Kufuatia hali hiyo serikali ya Rwanda kupitia msemaji wake akiwa pia waziri wa mashauri ya kigeni Dr Richard Sezibera amelaani kauli hizo akizitaja kama uzushi na upotoshaji kwa sababu hakuna sehemu hata moja ya Rwanda isiyo na usalama.

“Tafadhari msipoteze muda kwa taarifa hizi za uzushi zinazosambazwa na nchi jirani katika mitandao ya kijamii’’ amesema Dr Sezibera

Rwanda imekuwa ikisema kuwa Rwanda itahakikisha usalama wake na hakuna haja ya wageni au wananchi kuwa na wasiwasi kwa sababu nchi hiyo ni salama.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

Kigali: Mfanyakazi wa ndani amteka nyara mtoto wa miaka miwili  

Leki Aimat

Rwanda: Serikali yatangaza namna ya kutatua suala la uhaba wa simenti

kayre

Raisi ameomba ngazi za upelelezi kujua sababu gani Gen Kasirye Ggwanga kafyetua lisasi

Leki Aimat

Toa maoni