Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

RWANDA: QATAR NA RWANDA ZAZIDISHA USHIRIKIANO KWENYE SEKTA YA SHERIA

Mwanasheria mkuu wa Qatar Ali Bin Fatais Al Marri amesema mfumo wa sheria nchini Rwanda umepiga hatua nzuri ndani ya kipindi cha miaka 25 iliyopita kuliko ambavyo watu wanadhani.
Alikuwa akizungumza baada ya ziara yake katika makao makuu ya wizara ya sheria jijini Kigali ambapo alipata ufafanuzi kuhusu mabadiliko kwenye mfumo wa sheria za Rwanda na mchakato mzima wa jinsi sheria hizo zilizovyoendelea kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha zinakidhi mahitaji ya wananchi lakini pia kuendana na tunu zinazoongoza sheria za kimataifa.
Waziri wa nchi katika wizara ya sheria Uwizeyimana Evode ametoa ufafanuzi kuhusu mabadiliko hayo ikiwa ni pamoja na taasisi za kisheria zilizoanzishwa kama vile ofisi ya mtetezi wa umma na pia mamlaka ya taifa kuhusu upelelezi wa kisheria.
Kwa ujumla mwanasheria mkuu wa Qatar na ujumbe anaouongoza wamesema kwamba ziara yao ilitaka kufahamu mbinu za Rwanda kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi na ulaji rushwa.
@RwandaLeo

Maoni Husiano

RWANDA: WABUNGE WA AFRIKA WALALAMIKIA SERIKALI

Leki Aimat

Wengine 6 wa ajali ya moto wapoteza maisha

Leki Aimat

Mbinu 3 na Sheria 3 za kuteste muke hadi akupigie simu wa kwanza

Leki Aimat

Toa maoni