Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

RWANDA: RAIS KAGAME AWAASA VIONGOZI DHIDI YA UMASKINI

Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye anaendelea na ziara ya kikazi kwenye jimbo la magharibi mwa nchi hiyo amewaasa viongozi zaidi ya 600 katika jimbo hilo kuhakikisha wanapiga vita umaskini miongoni mwa wananchi.

Rais amesema kwamba jimbo hilo hupata bajeti ya faranga bilioni 120 kila mwaka na pesa hiyo lazima ilete mabadiliko katika maisha ya wananchi wa jimbo hilo.

Amewataka viongozi ngazi zote kufanya kazi kwa bidii na kwa pamoja ili kile kinachofanyika kiwe na tija kwa wananchi.

”Hilo ndilo ninahitaji tulizungumzie sisi kama viongozi, hatuwezi kufanya mambo tusipige hatua ni lazima tutazame mianya yote inayovuja ili kuhakikisha tunaiziba”Alisema Rais Paul Kagame

Alihoji iweje watu wawe na mzigo wa umaskini lakini washindwe kuutua pale wanapopewa nafasi ya kufanya hivyo.”Huwezi kuwa na mzigo wa umaskini, lakini ukipewa fursa ya kuutua unashindwa kufanya hivyo”

Amewaasa viongozi hao walioonekana kuwa makini na kusikiliza kauli zake kwamba ni jambo la kushangaza na la kusikitisha pale watu kutoka nje wanapokuja kutoa mafunzo ya jinsi wanyarwanda wanavyopaswa kupambana na utapiamlo, umaskini,n.k

”Huwezi kumtafuta mtu kuja kukufundisha ubaya wa umaskini, wakati wewe mwenyewe ukijua fika athari zake,tunawaona wataalam wakija hapa kutufundisha jinsi ya kupambana na umaskini, jinsi ya kutoa lishe bora kwa watoto wetu kwa nini tunakubali hayo?Alihoji Rais Kagame.

Amesema viongozi hawapaswi kuwa na tabia ya kusubiri kutekeleza wajibu wao, akawaasa kubadili fikra na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kwa mujibu wa kutatua shida za wananchi.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

58 WALAZWA HOSPITALI BAADA YA KULA SUMU HARUSINI

Leki Aimat

RAIS KAGAME AONGOZA KIKAO CHA SMART AFRIKA

Leki Aimat

UWAZI, MAWASILIANO NA TAKWIMU NI MSINGI-RAIS KAGAME

Leki Aimat

Toa maoni