Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

RWANDA: SHERIA ZA UKOLONI ZAPIGWA MARUFUKU

Bunge nchini Rwanda limepitisha mswada wa sheria inayolenga kuzifuta sheria zote zilizotungwa kabla na wakati wa ukoloni. Serikali ya Rwanda inasema inachukua uamuzi huo kutokana na kwamba sheria hizo zimepitwa na wakati na endapo zikiendelea kutumika zinaweza kuhatarisha mstakabari wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa wizara ya sheria ya Rwanda mswada huo unazihusu sheria zipatazo elfu moja ambazo bado zinatumiwa kwenye kitabu cha sheria za Rwanda huku zikiwa zimepitwa na wakati.

Rwanda ilipata uhuru wake tarehe mosi mwezi wa saba mwaka1962 kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji lakini serikali inasema ni ajabu mpaka sasa kuona bado kuna sheria iliyowekwa na mfalme Leopold wa pili wa Ubelgiji kuhusu Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambazo wakati huo zilikuwa chini ya himaya ya ukoloni wa kibelgiji.

Mswada huo umefikishwa mbele ya bunge na wizara ya sheria na bunge mara moja likaupitisha kwa kauli moja.

Waziri wa nchi kwenye wizara ya sheria akihusika na sheria na masuala ya katiba Evode Uwizeyimana akizungumza mbele ya wabunge amesema haya ni matokeo ya utafiti uliofanywa na wizara hiyo.

”Tulifanya utafiti kwenye sheria zetu na ni utafiti wa kina kwa sababu tulitaka kujua ikiwa kuzifuta haiwezi kutuathiri na baadaye kugundua kwamba sheria ambazo zilitungwa kabla na wakati wa ukoloni na ambazo tumekuwa tukizitumia zinafikia elfu moja. Sheria ya kwanza miongoni mwake ilitungwa mwaka 1885”Alisema waziri.

Waziri huyo akasema kwamba haikuwa ni busara kuendelea kuzikumbatia sheria hizo zikiwa na athari kwenye mfumo mzima wa sheria za Rwanda.

”Hatupendi kuendelea kufungwa na sheria za wakoloni tunazungumzia uhuru wa kisiasa tulioupata, na sasa tunaendelea na vita vya kupata uhuru wa kiuchumi. Sasa jambo lingine ni kuweka sheria zinazotufaa maana hiyo nayo ina uhusiano na uhuru kamili wa nchi”

Awali kikao cha baraza la mawaziri cha tarehe 3 mwezi wa nne mwaka huu ndicho kilichoidhinisha kwa kauli moja kuanzisha mchakato wa kufuta sheria zote za ukoloni kwenye mfumo wa sheria za Rwanda kwa madai kwamba hakuna uhuru kamili ikiwa bado nchi inakumbatia baadhi ya sheria za wakoloni kwenye sheria zake.

 

 

@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Russia yaendelea na mashambulizi ya anga

Leki Aimat

RWANDA: TALAKILISHI  400 ZAPOTEA BILA HABARI

Leki Aimat

DRC: Baada ya miezi 7 baraza la mawaziri latangazwa

Leki Aimat

Toa maoni