Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

RWANDA: SHULE ZA MSINGI ZA BWENI KUFUNGWA-WIZARA YA ELIMU

Wamiliki wa shule binafsi za msingi na wazazi kwa ujumla wameilalamikia hatua ya serikali ya Rwanda ya kufuta shule zote za bweni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2019. Serikali inasema hatua hii inanuia kuokoa maadili ambayo yaonekana kudidimia.

Awali uamuzi huu ulipitishwa na mwaka 2015ambapo liliziomba shule zote za msingi zilizokuwa na mfumo wa bweni kwa watoto wadogo kufuta mfumo huo mara moja. Wakati huo shule zote zilipewa kipindi cha miaka 3 kuridhia uamuzi huo wa baraza la mawaziri

Na sasa kauli ya wizara ya elimu ni kwamba mwisho wa mwaka huu kila shule iwe imekwishafuta kabisa mfumo huo. Ni suala ambalo hata hivyo limepokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wazazi

‘Barua tulizozipokea hapo awali zilituomba kutowasajili watoto chini ya miaka 10 hakuna barua iliyotutaka tuache kuwapokea watoto wanaosoma bweni. Hii ina maana kama nimewasajili watoto juu ya miaka 10 sijavunja sheria” Mmoja wa wamiliki wa shule hizo alilalamika.

Wamiliki hawa wa shule zenye mifumo ya bweni wamesema hawajafurahia uamuzi huo na kwamba mpaka sasa wamesalia kuwa bumbuwazi wasijue la kufanya hasa kutokana na kwamba baadhi walikuwa na mikopo benki.

Waziri wa nchi katika wizara ya elimu anayehusika na elimu ya msingi na sekondari Dr Isaac Munyakazi amesema kauli ya serikali inasalia kuwa ile ile isipokuwa kwa shule zitakazotuma maombi maalum kuonyesha nia isiyo ya kawaida ya kusalia na mfumo huo wa bweni kwa watoto wadogo.

”Hata yule atakayehitaji kusalia na watoto wenye umri juu ya miaka kumi atalazimika kutuma maombi maalum kufahamisha nia isiyo ya kawaida ya ni kwa nini anataka kuendelea na mfumo huo. Kwanza wanapaswa kujua kuwa kuwahifadhi watoto wadogo haikubaliki, sheria iko wazi. Tulichokuwa tumewakubalia ndani ya miaka 3 iliyopita tulisema kwamba kwa angalau wale wenye watoto juu ya miaka 10 walitakiwa kubaki nao mpaka tumejiridhisha kuwa hakuna wanafunzi wa bweni katika shule za msingi” alisema waziri.

Hatua hii pia imewagawa watu wenye maoni juu yake ambapo baadhi wanahisi ni hatua nzuri kwa sababu mtoto mdogo anatakiwa apate malezi kutoka kwa wazazi wake huku wengine wakisema kumpeleka mtoto mdogo bweni kunamsaidia kumuepusha tabia mbovu kutoka kwa wazazi ambao huishi pamoja bila kuelewana na ugomvi wa kila siku. Kuna wengine wanaodhani kuwa kumpeleka mtoto mdogo bweni kunamteganisha na maadili ya kinyarwanda suala ambalo pia wizara ya elimu inaliunga mkono.

Uamuzi huu unazihusu shule za msingi zenye mfumo wa bweni zipatazo 66 ambazo kabla ya kumalizika mwaka huu zinatakiwa kuwa zimefunga milango yake.

 

@Rwanda Leo

Maoni Husiano

RWANDA: MAJENGO KWENYE MABONDE YAANZA KUBOMOLEWA

Leki Aimat

Rimba: raia wanahitaji mkusanyiko wa wazazi urudishwe

Leki Aimat

Kigali: Mvulana na ndugu ye wa kike waka nje wiki mbili baada ya nyumba yao kubomolewa

Leki Aimat

Toa maoni