Rwanda Leo
Image default
HABARI SLIDE

RWANDA: TALAKILISHI  400 ZAPOTEA BILA HABARI

Taarifa kutoka wizara ya elimu zimefahamisha kwamba jumla ya talakilishi ndogo za mkononi ama kompyuta zimepotea katika mazingira ya kutatanisha kwenye jimbo la kusini nchini Rwanda.

Katika kikao na viongozi wa jimbo la kusini waziri wa nchi katika wizara ya elimu Dr Isaac Munyakazi amesema kwamba pamoja na kupotea kwa talakilishi hizo washukiwa wanaendelea kushikiliwa.

Talakilishi zilizopotea ni zile za mradi wa kitaifa maarufu kama“one per child” waziri ameonya kwamba wanaojaribu kuhusika katika kupotea kwa talakilishi hizo ambazo kimsingi zililetwa kusaidia mkakati mpana wa serikali wa kujenga uchumi unazingatia sayansi na teknolojia hawatavumiliwa.

Amesema serikali haitakosa kuwafuatilia hadi wakabiliwe ipasavyo.Huku akibaini kuwa baadhi ya wanaoshukiliwa kwa kushukiwa ni walinzi wa shule zilikoibiwa kompyuta hizo.

Wilaya ya Muhanga ndiyo ilipoteza kompyuta nyingi kwa kuwa  180 kati ya zilizoibwa zote ziliibiwa wilayani humo.

Mradi wa one laptop per child ulianzishwa na serikali ya Rwanda mwaka 2000 ili kusaidia utekelezwaji wa mkakati wake mpana wa kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa na talalikilishi yake kuanzia shule za msingi ili mwishowe kuwepo na watalaam wanaoweza kuimarisha uchumi wa nchi hiyo kwa kuzingatia sayansi na teknolojia.

 

Munyarugendo20@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Centre Africa: Serikali  na Wapinzani wake wamesaini makubaliano ya amani

Leki Aimat

RWANDA: QATAR NA RWANDA ZAZIDISHA USHIRIKIANO KWENYE SEKTA YA SHERIA

Leki Aimat

RWANDA: MAJENGO KWENYE MABONDE YAANZA KUBOMOLEWA

Leki Aimat

Toa maoni