Rwanda Leo
Image default
SIASA SLIDE

RWANDA: UCHORAJI VIBONZO DHIDI YA MKUU WA NCHI KOSA LA JINAI

Mahakama kuu nchini Rwanda imetupilia mbali shitaka lilokuwa limetolewa na baadhi ya wanasheria nchini kupinga sheria iliyoanzishwa mwaka jana kuwa ni kosa la jinai kuchora vibonzo vinavyomkejeli Rais wa nchi hiyo .Wakati huo wanasheria hao walianzisha kesi kulipinga hilo huku wakisema hiyo ilikuwa ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Kuanzishwa kwa sheria hiyo pia kulizua malalamiko mengi kutoka kwa waandishi wa habari wakitaja kuwa kuwepo kwa sheria hiyo kulihatarisha uhuru wao wa kufanya kazi katika mazingira huru zaidi.

Sasa mahakama kuu imetoa hukumu ambayo inasema kuwa kuchora kibonzo kinachomkejeli Rais kwa njia yoyote ile liendelee kuwa kosa la jinai.Huku pia kosa la ubakaji na uasherati wa aina yoyote ile likiendelea pia kuwa la jinai kwa mujibu wa uamuzi huo.

Hata hivyo mahakama hiyo imeamua kuwa viongozi wengine waandamizi serikalini na pia viongozi wakuu wa madhehebu ya dini wao kuwachora kwenye vibonzo halitakuwa kosa la jinai.

Mkuu wa jopo la majaji waliokuwa wameishitaki serikali kuhusu sheria hiyo Richard Mugisha akizungumza kwa niaba ya wenzake amesema wao kama wanasheria wameridhika na uamuzi huo kwa sababu wasingetoa shitaka lao hata hivyo vipengere vingine visingeondolewa kwenye sheria hiyo.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

Kigali: Ashtakiwa Kumbaka Mwenye Ulemavu Wa Akili

Leki Aimat

Raia wa Tumba wanaitaka serikali kuwapatia nguzo za umeme

Leki Aimat

Waliojeruhiwa Somalia wasafirishwa

Leki Aimat

Toa maoni