Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SIASA SLIDE

RWANDA: WABUNGE WA AFRIKA WALALAMIKIA SERIKALI

Serikali za mataifa ya Africa zimehimizwa kuweka mikakati na sheria mahsusi zinazompa mwanamke mamlaka na haki sawa na mwanaume kuhusu umiliki wa ardhi.Ni kauli iliyotolewa jijini Kigali na wabunge kutoka kanda za Afrika mashariki na magharibi kuhusu jinsi ya kumwinua mwanamke kwenye nyanja mbalimbali

Takwimu zilizotolewa kwenye mijadala hii zimeonyesha kwamba asilimia50% ya wanawake kusini mwa jangwa la sahara wanajihusisha na shughuli za kilimo.Lakini jambo lilibainika ni kwamba wengi wa wanawake hao wanaishi kwenye umaskini wa kupindukia wakati ndiyo wazalishaji wakubwa kwenye sekta ya kilimo.

Christopher Bazivamo naibu katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki akafafanua

Kuna baadhi ya mataifa ambapo unakuta kuwa hata kama mwanamke ndiye mwendeshaji mkuu wa shughuli za kilimo lakini hana nafasi kwenye umiliki wa ardhi,unakuta haki hiyo ni ya mwanaume peke yakeAmefafanua

Changamoto hii ni mojawapo ya mambo yanayojadiliwa kwenye mkutano wa siku nne unaoendelea mjini Kigali kuhusu haki za wanawake kwenye uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.Na mikakati inayotazamiwa kuazimiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wanawake kwenye nyanja mbalimbali.

Mwakilishi mkazi wa shirika la chakula ulimwenguni FAO Dr Gualbert Gbèhounou  ,ametaja athari za kushindwa kukabiliana changamoto hii

”Ili muelewe athari za tatizo,nataka niwakumbushe kuwa mwaka 2017 watu milioni 821 walikosa chakula, na wengine wapatao bilioni moja waliugua magonjwa yaliyosababisha na ukosefu wa lishe bora, na mamia ya wengi hutembea na njaa”Alionya

Nchini Rwanda kwa mfano takwimu za taasisi ya taifa kuhusu takwimu zinaonyesha kuwa sekta ya kilimo huchangia asilimia 29% ya pato zima la taifa.

Wajumbe wa mkutano huu ni wabunge kutoka mabunge ya nchi za jumuiya ya Afrika mashariki EALA,wale kutoka nchi zinazounda jumuiya ya afrika magharibi ECOWAS na hata wabunge la Rwanda.Wote kwa kaulimoja wanasema bila kuzingatia usawa na kijinsia mafanikio ya kukomesha changamoto hizo yataishia patupu.

 

@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Rwanda:Bwana arusi amuacha mkewe kanisani akakimbia

Leki Aimat

Uganda yamruhusu mkuu wa MTN kurejea nchini

Leki Aimat

Rwanda: Mwanamke asema alivyofanya Nchini Kuwait

Leki Aimat

Toa maoni