Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

RWANDA YATHIBITISHA KUMKAMATA SANKARA

Kwa mara ya kwanza Rwanda imekiri kumshikilia msemaji wa waasi wa makundi yanayoendeshea harakati zao nje ya nchi kuhujumu utawala wa Kigali. Msemaji wa serikali ya Rwanda Dr Richard Sezibera amethibitisha taarifa hizo wiki mbili baada ya kuwepo uvumi kuwa huenda muasi huyo alitiwa mbaroni.

Taarifa za awali zilisema kuwa Calixte Nsabimana almaarufumajor Sankara  zilisema kuwa alikamatwa kwenye visiwa vya Comoros wiki mbili zilizopita.

Wakati huo wanachama wenzake walikanusha habari hizo wakisema zilikuwa ni upotoshaji.Hata hivyo kuanzia wakati huo Sankara ambaye kila mara alisikika kwenye vyombo vya habari vya kimataifa akijigamba mashambulizi eneo la magharibi mwa Rwanda hakusikika tena hali iliyopelekea wengi kujiuliza kulikoni.

Dr Richard Sezibera

Hata hivyo mapema leo akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigali waziri wa mashauri ya kigeni na msemaji wa serikali ya Rwanda Dr Richard Sezibera amevunja ukimya na kuutangazia ulimwengu kuwa mshukiwa yuko mikononi mwa vyombo vya sheria vya Rwanda.

”Huyu anayejiita major Calixte Sankara ambaye mmekuwa mkimsikia akijitapa kufanya mashambulizi mbalimbali yaliyotokea eneo la magharibi mwa nchi, ambayo yaligharimu maisha ya raia wetu eneo la Kitabi,tunaye na tunajiandaa kumfikisha kizimbani kjibu tuhuma dhidi yake” Alisema Dr Sezibera

Kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari waziri wa mashauri ya kigeni Dr Sezibera alikuwa amekutana kwa faragha na wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao nchini Rwanda na kuwafafanulia kero ya serikali ya Rwanda hasa linapokuja suala la kushughulikia wale wote ambao Rwanda inawatuhumu kuhujumu utawala wake.

”Kuna hawa watu wanaoishi nje ya Rwanda ndani ya mataifa hayo baadhi hadi wana uraia wa mataifa na wanatembea hapa na pale raha msitarehe, bila bughudha na wanaendesha harakati zao ndani ya nchi hizo, huku mataifa haya yakijua wazi kuwa watu hawa wana kesi za kujibu nchini Rwanda.Tumesema mienendo hii hakubaliki kamwe” Alionya waziri

Rwanda imesema mara zote kuwa iko chonjo juu ya usalama wake na imekuwa ikionya yeyote anayejitwisha jukumu la kuhujumu usalama wake.

Major Sankara

”Siyo huyu peke yake, hata wengine ambao wanaendelea kuhujumu usalama wetu, wakifanya mauaji ya raia wetu wakiwa nje siku moja watajibu vitendo hivyo” Aliendelea kuonya msemaji wa serikali

Callixte Sankara alikuwa ni msemaji wa kundi lililojiita P5 linaloyaunganisha makundi matano yanayopambana dhidi ya serikali ya Rwanda.Mpaka sasa wakereketwa wenzake bado kutanagaza chochote na licha ya wananchi kukataa kulizungumzia suala hilo wengi kwenye mitandao ya kijamii walionekana kupongeza hatua ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo ambaye kila mara amekuwa akiapa kuung;oa madarakani utawala wa Rwanda kwa mtutu wa bunduki.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

RWANDA: TALAKILISHI  400 ZAPOTEA BILA HABARI

Leki Aimat

RWANDA: SHULE ZA MSINGI ZA BWENI KUFUNGWA-WIZARA YA ELIMU

Leki Aimat

KUWENI MFANO BORA-KAGAME AYAASA MAJESHI

Leki Aimat

Toa maoni