Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SIASA SLIDE

Rwanda yawasilisha ombi la DRC kuingia EAC

Rwanda imewasilisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuingia katika muungano huu.

Muungano wa EAC kwa sasa unaundwa na nchi sita ambazo ni:  Rwanda, Tanzania, Uganda, South Sudan, Kenya na Burundi.

Waziri Makamu wa Mambo ya nje husika na EAC, Olivier Nduhungirehe kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “ Barua ilipokewa na kuwasilishwa kwa Katibu tarehe 13 Juni.”

Hilo, ni baada ya Rais wa DRC, Felix Tshisekedi Tshilombo kumuandikia mwenzake wa Rwanda, Kagame akiomba kuingia katika EAC.

Somalia pia iliomba hili lakini haijakubaliwa bado.

 

@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Ninyi ni uzao wa nyoka, maneno huonyesha hali ya moyo

Leki Aimat

MAFUNZO KWA VIONGOZI WAKUU-RWANDA

Leki Aimat

Eden Hazard amemaliza safari yake na klabu ya Chelsea

Leki Aimat

Toa maoni