Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SLIDE

Rwanda: Baada ya kuadhibiwa na kanisa Katolika Padri afunga ndoa

Padri  Cesar Serinda ameoa baada ya kanisa katoliki nchini Rwanda kumpiga marufuku kuendelea na kazi zake za kitume.

Habari tunazo pokea  kwenye mitandao ya kijamii nchini humo, ni kwamba Serinda alioa juma pili iliyopita.

Makamu  Askofu wa Diosisi ya Butare, Mgr Musenyeri Jean Marie Vianney Gahizi, amesema hajajua mengi kuhusu taarifa hizo lakini amehakikisha Padri Serinda alikomeshwa madarakani kutokana na tabia zake za uruka njia.

Alisimamishwa kazi kutokana na tabia zake potovu mwaka jana 2018.

” Hii si mara yake ya kwanza ama ya pili kupewa onyo. Nimepokea picha zake kama anakula kiapo, lakini siwezi kuhakikisha kwamba ni ukweli. Siwezi kushangaa kwa hilo.”

Askofu Gahizi amesema kuwa padri huyo alizaa watoto kwa wanawake  wawili tofauti. Haya ni kwa mujibu wa gazeti bwiza limeandika.

 

@RwandaLeo

Maoni Husiano

ASILIMIA 24% YA WAAFRIKA HUTUMIA INTERNET

Leki Aimat

GICUMBI: WAWILI WAPOTEZA MAISHA

Leki Aimat

RWANDA YATHIBITISHA KUMKAMATA SANKARA

Leki Aimat

Toa maoni