Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI JIFUNZE KISWAHILI SLIDE

Tanzania: Wajumbe wa Rwanda kwenye mkutano wa Umoja wa Africa (ACALAN) Kiswahili

Wiki iliyopita Dar Es Salaam -Tanzania kumemalizika mkutano wa kitengo cha Umuja wa Africa ( AU) kinacho husika na maswala ya kukuza na kuendeleza lugha za  Kiafrica ( ACALAN)  .

Waliyohudhuria mkutano huo ni watalaamu  mbalimbali kutoka asasi na mashirika ya kikanda na kimataifa ikiwa ni pamoja na  UNESCO, ACALAN,  EAKC , CHAUKIDU na mengine mengi,  vyuo vikuu,  watafiti n.k kutoka Africa mashariki na Kati.

Madhumuni ya mkutano huo ni kutafuta mikakati,  ushirikiano na utangamano wa karibu na mwafaka ili kukuza Kiswahili Kama lugha ya mwafrika kwa mawasiliano mapana barani Africa na Ulimwengu mzima.

Wajumbe kutoka Rwanda

Wajumbe kutoka Rwanda: Professor Niyomugabo Cyprien, Dk Vuningoma James, Nibakwe Edith, Nshimyumukiza Janvier Popote pakiwemo pia Professor MALONGA ambaye ni Mwenyekiti  wa Kamati ya Uhusiano na Ushirikiano ya Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani ( CHAUKIDU)  alitujulisha kwamba kuna kongamano la Chama hicho mwezi  Disemba huko Chuo kikuu cha Kyambogo – Uganda  na watu wengi wapenzi na wadau wa Kiswahili wameonyesha nia na hamu kubwa kuona kongamano la kimataifa kama hilo likifanyika Kigali mwakani 2020.

 

@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Rais Kagame aeleza mwelekeo mpya wa ushirikiano na Ufaransa

Leki Aimat

Rwanda: Waziri wa sheria kapigwa faini na trafiki

Leki Aimat

DRC: YAIGA RWANDA KWENYE USAFI

Leki Aimat

Toa maoni