Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SIASA SLIDE

Uganda yamruhusu mkuu wa MTN kurejea nchini

Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya MTN ambayo imekuwa ikifanya biashara zake nchini Uganda ameruhusiwa kurejea nchini.

 Afisa wa kampuni hiyo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa amri hiyo ya kufuzwa kwake imedumu kwa zaidi ya miezi mitatu.

Wim Vanhelleputte, Mtendaji Mkuu wa MTN Uganda, alifukuzwa kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki Februari 15, 2019, kwa sababu za usalama wa taifa, polisi walisema wakati huo, bila ya kutoa maelezo zaidi.

“Tumejulishwa rasmi, tumepata barua na ilikuwa ni rais ndiye alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani kutuandikia na kumruhusu mtendaji wa MTN kurejea haraka nchini na hivyo atawasili hivi leo,” amesema mwenyekiti wa MTN Uganda, Charles Mbire.

Amesema Vanhelleputte huenda akaanza shughuli zake kama mkuu wa kampuni.

Maendeleo haya ni dalili ya kwanza ya kurejea kwa uhusiano mwema kati ya kampuni na serikali ya rais Yoweri Museveni, kufuatia shutuma kuwa mtandao wa kampuni ulijihusisha na shughuli za kijasusi na kukwepa kodi, miongoni mwa masuala mengine.

 

@Rwandaleo.com

Maoni Husiano

Rwanda: Akamatwa na madawa ya kulevya

Leki Aimat

Raia wa Tumba wanaitaka serikali kuwapatia nguzo za umeme

Leki Aimat

Mgonjwa aliyelazwa miaka 20 amebakwa na kutwikwa mimba

Leki Aimat

Toa maoni