Rwanda Leo
Image default
AFYA BURUDANI HABARI KTK PICHA HABARI KWA UFUPI HADITHI MAONI MICHEZO SIASA SLIDE VISA

Uhaba wa maji wajitokeza kaskazini mwa Rwanda

Wakazi wa wilaya ya Gicumbi, kaskazini mwa Rwanda wametangaza kukabiliana na suala la uchache wa maji kiasi  wananunua dumu moja la maji frw 300-400.

Wakazi wamesema uhaba wa maji umekumba karibu tarafa zote  wilayani hasa  Rukomo, Rutare, Ruvune na Rwamiko. Hawa wamesema licha ya kuwa na maji hapo awali, sasa wamekosa na hawajui yamekosekana kivipi.

Kujibu hilo, mamlaka ya wilaya hii inatangaza  kumekuwa na shida la mtambo ambao ulikuwa ukiyasukuma maji hayo,  hivi akiahidi kuwa soko la kununuwa mashine  nyingine limeshawekwa mnadani na maji safi yataonekana hivi karibuni.

Suala hili limezusha   malalamishi ya wakazi  kuwa watoto wengi wilayani humo, wanachelewa kuenda shuleni huku wengine wengi wakiacha shule na kuwa  hili limeathiri kilimo kwani muda mrefu tu wanaupoteza wakitafuta maji badala ya kufanya kazini nyingine.

Takwimu kutoka mkoa wa Kaskazini zinaonyesha wilayani Musanze tu ndiko kunakojitoshereza kwa maji safi, ikifuatiwa na Rulindo ambayo inamiliki maji kadri ya 90%, huku wilaya hii ya Gicumbi ikiburuta mkia kwa umiliki wa maji unaokadiriwa kuwa chini ya 50%

Maoni Husiano

RWANDA: WABUNGE WA AFRIKA WALALAMIKIA SERIKALI

Leki Aimat

Abdel Fattah al-Sissi, mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika

Leki Aimat

Rwanda: Serikali yatangaza namna ya kutatua suala la uhaba wa simenti

kayre

Toa maoni