Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

USALAMA WAHITAJI USHIRIKIANO-INTERPOL

Kongamano la kikanda kuhusu usalama lililowajumuisha pamoja maafisa wa usalama kutoka polisi wa kimataifa Interpol limekamilishwa jijini Kigali Rwanda.

Zaidi ya wa wajumbe 300 walikusanyika kwa muda wa siku tatu na mwishoni mwa kongamano lao wakaomba kuwepo mtandao wa ushirikiano katika kutokomeza visa vinavyovuka mipaka.

Waziri wa sheria wa Rwanda akiwa pia mwanasheria mkuu wa nchi hiyo Johnston Busingye aliyefunga rasmi kongamano hilo aliwaambia wajumbe hao kuwa ushirikiano kwenye mapambano ya visa na makosa yanayofanywa kwa ustadi wa kisasa ni suala ambalo mpaka sasa limesalia kuwa jukumu muhimu miongoni mwa wadau wa usalama karibu kwenye ngazi zote.

Mojawapo ya maazimio makubwa yaliyochukuliwa,ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha ngazi zote za usalama barani Afrika zinaweka mtandao mmoja wa kupeana taarifa za ujasusi kuhusu kukomesha visa vinavyohatarisha usalama wa mataifa hayo.

Waziri wa sheria wa Rwanda aliwapongeza viongozi wakuu wa polisi kutokana na kile alichokitaja kama juhudi za maksudi za kuhakikisha usalama.

”Tunawapongeza wakuu wa polisi na wakuu wa taasisi nyingine husika ulimwenguni kutokana na juhudi zenu za kila mara za kuhakikisha usalama kwenye bara letu” alisema Busingye

Aidha aliongeza kusema kwamba thamani ya kongamano hilo ambalo alilitaja kama fursa muhimu kwa wadau kukutana pamoja na kujadiliana mikakati mikali ya usalama itakuwa muhimu kwa matarajio yajayo.

Kongamano la aina hii hufanyika kila baada ya miaka miwili ili kutathmini hali ya usalama na ushirikiano miongoni mwa wadau katika ngazi za usalama.

 

RwandaLeo

Maoni Husiano

Nyamagabe: Mto wa Mushishito huharibu mavuno ya wakulima

Leki Aimat

Prof.Sam Rugege aomba wazalendo wa Nyagatare kuonyesha mikono yao ili rushwa imalizike

Leki Aimat

RWANDA: MIKUTANO YA KIMATAIFA  CHACHU YA MAENDELEO

Leki Aimat

Toa maoni