Rwanda Leo
Image default
HABARI SIASA SLIDE

UWAZI, MAWASILIANO NA TAKWIMU NI MSINGI-RAIS KAGAME

Rais Paul Kagame amesema kwamba imani,mawasiliano na takwimu za uhakika ndiyo msingi maridhawa wa kuhakikisha vita dhidi ya magonjwa ya milipuko yanakabiliwa ipasavyo. Rais Kagame alikuwa akizungumza kwenye kongamano la kimataifa kuhusu usalama lililofanyika jijini Munich nchini Ujerumani.

Kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka na kujumuisha marais na wakuu wa serikali mbalimbali ulimwenguni limekuwa ni jukwaa la kutafuta michango ya majadiliano yanayolenga kutafuta suluhu la changamoto zinazowakabili wakazi wa ulimwengu kwenye sekta ya usalama na amani.

Rais Kagame akasema ‘’Milipuko ya Ebola kwa mfano miaka iliyopita,iliyotokea kwenye nchi ambazo kimsingi zilikuwa na usalama magharibi mwa Afrika iliathiri sana,kinyume na hali ya kawaida ule mlipuko wa ebola uliotokea mashariki mwa DRC umeweza kudhibitiwa licha ya ukweli kwamba kwenye eneo hilo usalama ni wasiwasi.Lakini tofauti ni kwamba matabibu mashariki mwa DRC wana uzoefu wa kuyakabili mambo na yumkini wanaelewana na raia wa eneo hilo.Lakini magharibi mwa Afrika ugonjwa huo ulichukua miezi kadhaa kabla ya kutambuliwa na kupelekea hasara ya mabilioni ya pesa’’ Alisema Rais Kagame.

Akizungumzia utayari wa Rwanda katika kupambana na magonjwa ya milipuko Rais Kagame alisema serikali ilifanya kila jitihada za kuweka mikakati ya kupambana na hali yoyote ya milipuko

‘’Nchini Rwanda tuna washauri nasaha na wafanyakazi wa afya wapatao elfu 60  waliosambazwa kote nchini, hii inaisaidia serikali kutambua magonjwa zaidi ya 23 ya milipuko kila siku kwa kutumia teknolojia’’ Alisema Rais Kagame

Kongamano hili linatazamiwa kukamilishwa kwa kuchukua mikakati endelevu itakayosaidia kukabiliana na tatizo la usalama mdogo.

 

@Rwandaleo

Maoni Husiano

Cyarwa: raia waangamizwa na maradhi ya matekenya

Leki Aimat

RWANDA: WABUNGE WA AFRIKA WALALAMIKIA SERIKALI

Leki Aimat

China haitaruhusu ndoa za watu wa jinsia moja

Leki Aimat

Toa maoni