Rwanda Leo
Image default
HABARI HABARI KWA UFUPI SIASA SLIDE

WAKIMBIZI WA LIBYA WAWASILI RWANDA

Kundi la pili wakimbizi wahamiaji  wa kiafrika kutoka Libya limewasili nchini Rwanda usiku wa kuamkia leo.Kundi hili la watu 123 limekuja wiki moja baada ya kundi la kwanza la wahamiaji 66 kuwasili Rwanda kutoka Libya. Idadi hii imewafanya wakimbizi wahamiaji kutoka Libya hadi Rwanda kufikia watu 189

Miongoni mwa waliowasili usiku wa kuamkia jana ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi miaka 20. Wizara inayohusika na majanga na huduma kwa wakimbizi nchini Rwanda imesema kwamba inaendelea kuwahudumia wakimbizi hao na kwamba hadi sasa hakuna kisa ambacho kimetokea na wahamiaji wote wako katika hali nzuri.

Rwanda inatazamiwa kuwapokea wahamiaji wakimbizi wa kiafrika kutoka Libya wapatao mia tano. Rais Paul Kagame wa Rwanda alisema wiki hii kwamba ijapokuwa Rwanda haina uwezo wa kutosha lakini inafanya hivi kutokana na moyo wa kukosa uvumilivu kuwaona vijana wa kiafrika wa kiafrika wakiendelea kuteseka kwenye maisha magumu kwenye safari hii hatari ulimwenguni ya kujaribu kuvuka kwenda Ulaya.

 

Rwandaleo

Maoni Husiano

Ninyi ni uzao wa nyoka, maneno huonyesha hali ya moyo

Leki Aimat

Prof.Sam Rugege aomba wazalendo wa Nyagatare kuonyesha mikono yao ili rushwa imalizike

Leki Aimat

Wengine 6 wa ajali ya moto wapoteza maisha

Leki Aimat

Toa maoni